Waziri Mwijage Afunguka Baada JPM Kutoridhishwa na Utendaji Wake
Jana (August 6, 2017) Rais Magufuli
alitoa kauli ya kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na
kuvitelekeza ambapo alimtaka Waziri Mwijage kuwanyang’anya na kuwapatia
wawekezaji watao viendeleza.
Leo August 7, 2017 Waziri wa Viwanda
Charles Mwijage amehojiwa kwenye Clouds 360 Clouds TV na kuelezea kuhusu
hiyo kauli ya rais na kutoa hizi kauli.
”Kujenga viwanda sio mchezo, yapo
maelekezo ya Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe,
Rais alichokitegemea kwangu sio kile anachokiona sababu viwanda haviendi
kwa kasi anayoiona na hii kuna sababu kadhaa.
“Hii sekta ya viwanda ni
multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, vingine
maliasili…. kuna viwanda vimechukuliwa lakini havipo kwenye orodha ya
viwanda vilivyobinafsishwa, nahitaji Wakuu wa mikoa waingie hapa.
“Kuna watu wengine wameingia
kwenye sekta ya viwanda lakini hawajui shughuli yake wengi
wanang’ang’ania faida tu…. moja ya masharti ya viwanda watu walitakiwa
kuviendeleza lakini kuanzia Ijumaa mimi nitaanza kutenda bila kuwa na
maneno.
“Suala la kiwanda cha Mang’ula
tayari mgogoro wake umefika Bungeni na mmiliki wake tayari ameitwa
Bungeni kuhojiwa, kiwanda cha matairi Arusha tumekiongezea nguvu lakini
tunahitaji muwekezaji ataekuwa na nguvu zaidi kwenye uzalishaji.
“Kiwanda cha General Tyre kina
historia kubwa zaidi kilikuwa cha jumuiya ya Afrika Mashariki lakini
sasa ni mali yetu, siwezi kumsemea Mh Rais najua ana imani na mimi sana
ndio maana nilimuomba asinikumbushe tena siku nyingine.
“Anayetaka kujua viwanda vingapi
vipo mkoa wa Pwani aanzie mkuranga mpaka zegereni kuna zaidi ya viwanda
20 hapo, kiwanda cha Mgololo mufindi kinafanya kazi lakini kuna baadhi
ya shughuli nyingine za uzalishaji zinaendelea nje ya nchi.” Amesema Waziri Mwijage
Comments
Post a Comment