Posts

RAIS MUSEVENI AWASILI JIJINI TANGA TAYARI KWA SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI HAPO KESHO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (haonekani pichani) na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani. Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.

HUU NDIO MUONEKANO WA MFANYABIASHARA YUSUPH MANJI LEO MAHAKAMANI

Image
   August 4,2017 Upande wa serikali umewasilisha pingamizi la awali Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Yusuf Manji. Pingamizi hilo limewasilishwa leo na wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Naibu Msajili, Sian Mustafa kutokana na Jaji Isaya Arufan anayesikiliza maombi hayo kutokuwepo. Katika pingamizi hilo, wakili Kadushi amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana ya Manji. Pia kiapo kilichowasilisha cha kuhusu dhamana kinadosari kisheria, pamoja na kuwepo kwa vifungu visivyo sahihi. Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Msajili Mustafa ameahirisha kesi hiyo hadi August 7/2017 kwa ajili ya kusikilizwa. millardayo.com  imezinasa picha hizi ambazo zinamuonesha Mfanyabiashara Yusuph Manji akiwa amefuga ndevu ikiwa ni tofauti na ambavyo amekuwa akionekana.                  

Polisi limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu kwa wafanyabiashara wa TV, Simu na Computer “USED”

Image
Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu ijayo kwa wafanyabiashara na wauzaji wa television,Computer na simu za Mkononi zilizotumika maarufu Used’ baada ya kubaini katk maduka hayo kumekuwa maficho ya mali zinazoibiwa katika maeneo mbali mbali jijini dsm. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Kaimu Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dsm Lucas Mkondya amesema katika miezi ya hivi karibu kumeibuka wizi wa Uvunjaji majumbani ambao wahalifu huchuku Tv hasa zile Flat screen ambapo jeshi hilo limebaini hupelekwa katika maduka hayo. Jeshi hilo pia litawakamata watu wote wanaoendesha biashara ya magari yasiokuwa katika yard katika maeneo ya jiji la Dsm. Aidha jeshi hilo pia kuanzia jumatatu litaendesha Msako wa Kukamata magari yote yenye Vioo vyeusi maarufu TINTED baada ya kubaini kuwa baadhi ya wahusika hujihusisha na Uhalifu na Uporaji,kuficha mali za wizi lakini pia kufanyia vitendo visivyofaa vya Uzinzi. Akizungumzia matukio y

Wanaomuua Jini Kabula Wajulikana!

Image
WAKATI hali ya staa wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ikiwa bado si shwari, watu ambao wanatajwa kuzidi kumuweka kwenye wakati mgumu na kumsukumizia kwenye kifo wamejulikana, Ijumaa linakupa habari hii ya kusikitisha. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Jini Kabula anayedaiwa kuwa na tatizo la kuchanganyikiwa, alisema anashangaa wakati yuko kwenye matatizo hayo mazito ndipo ndugu na marafiki zake wanamtenga, hali ambayo inaweza kukatisha uhai wake. Alisema anapitia kwenye changamoto nzito kimaisha ambapo anahitaji msaada kutoka kwa watu wake wa karibu lakini kinachomsikitisha ni kwamba, anakimbiwa na kupewa kila aina ya jina baya likiwemo la kuitwa kichaa. “Nimeteswa na kuumizwa sana, eti mimi naitwa kichaa, kweli mimi naweza kuwa kichaa, ama kweli hii dunia ni katili sana na kwa hali hii nitakufa. “Naomba ifahamike kwamba nina matatizo makubwa sana, napitia mateso mazito, nimetengwa na watu wananikimbia, hata wale ambao tulikuwa tunasaidiana

KINANA AWASILI TANGA KUSHIRIKI UZINDUZI WA UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu baada ya kuwasli kwenye mkutano wa hadhara wa Rais Dk. John Magufuli uliofanyika katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, leo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mwanasha Tumbo  Mbunge wa  Viti Maalum mkoa wa Tanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu akisalimia wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakati wa mkutano huo  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akienda jukwaani kusalimia wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Rais Dk Magufuli  Katbu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza alipoalikuwa kuzungumza wakati wa mkutano huo.  Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo  Mke wa Rais Mama Janet Magufuli akisalimia kwenye mkutano huo  Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine wa meza kuu akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahm

HATIMAYE Aliyekuwa MKE wa Mbunge Sugu Faiza Ally Apata Mtoto Mwingine

Image
Leo ipo good news inayomuhusu Faiza Ally baada ya kujifungua salama mtoto. Kupitia Instagram yake leo August 3, 2017 Faiza Ally amethibitisha kuwa amebahatika kujifungua mtoto, akiweka picha ya mtoto huyo na kuweka maneno ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuandika>>>”ALHAMDULILLAH @lijunior_well come to the world baby

CUF Wazichapa Kavukavu Mahakama Kuu ya Tanzania DSM

Image
Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba na wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif, wamezichapa konde Mahakama Kuu Kanda ya Dar leo wakati wa kesi ya wabunge waliofutwa uanachama  Aidha wabunge hao waliiomba mahakama kuzuia utekelezaji wa Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kuwavua uanachama. Kesi hiyo inatarajiwa kutolewa uamuzi leo amahakamani hapo.

Msitumie hati ya kusafiria kama kitambulisho

Image
Idara ya Uhamiaji nchini imewataka wananchi kutambua kuwa paspoti siyo kitambulisho ndani ya nchi na kwamba kisitumike kwa matumizi hayo kwa sababu siyo utaratibu uliopangwa kisheria ndani ya mipaka ya nchi. Pia amesema kuwa ikibainika kuwa mtu amepoteza paspoti hiyo kizembe hatopewa nyingine. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga wakati alipofanya mahojiano maalumu na gazeti hili, na kuwaomba wananchi kutambua kuwa paspoti zinazotolewa zinapaswa kutunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa la kusafiria nje ya nchi. Kihinga alisema kumekuwa na maombi ya kutengenezewa paspoti baada ya kupotezwa, lakini wengi wamekuwa wakitoa sababu ambazo zinatilia shaka umakini wa mtu kwenye utunzaji wake. “Naomba mfahamu kuwa paspoti pia zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi hivyo visitumike kama vitambulisho na tena si vizuri kutembea nayo kila mahali kama huna safari ya nje ya nchi. Paspoti au hati ya kusafiria z

MARUBANI WAKIONA CHA MOTO BAADA YA KUMRUHUSU MTOTO KURUSHA NDEGE

Image
Serikali nchini Algeria, imewafukuzwa kazi marubani wawili wanaofanya kazi katika shirika la ndege la serikali baada ya kumruhusu mtoto wa miaka 10 kuendesha ndege. Mtoto huyo anayedaiwa kuwa ni yatima alikuwa akiendesha ndege aina ya Air Algerie, iliokuwa na abiria ndani na ilifanya safari zake katika mji wa Algiers hadi Setif. Zoezi la mtoto huyo kuendesha ndege lilifadhiliwa na kurekodiwa kituo cha El Bilad TV, ambapo walionyesha tukio zima huku kijana huyo akiwa amevalia sare za rubani. Baada ya video na picha kusambaa za kijana huyo akiongoza ndege, ndipo serikali ilichukua hatua ya kuwafukuzwa kazi Marubani hao mnamo Julai 29 mwaka huu.

Tambua Madhara ya Ulaji wa Chipsi

Image
Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree. Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini. Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari. Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana

ATCL WATANGAZA NAFASI ZA KAZI 24, AUGUST 2017

Image
Air Tanzania Company Limited (ATCL) is in the process of revamping its operations and has introduced new equipment to its fleet. In line with this expansion, the Company hereby invites the applications from qualified Tanzanians to fill following positions:-       1. POSITIONS: 1.1 DIRECTOR OF FINANCE AND ADMINISTRATION REPORTS TO: MANAGING DIRECTOR &CHIEF EXECUTIVE OFFICER SUPERVISES: Sections under Finance and Administration Department JOB SUMMARY: Provide advisory services to the Accounting Officer in the proper management of Company’s resources. MINIMUM ENTRY QUALIFICATIONS A minimum of a Bachelor Degree in Accounts/Finance with a (CPA) (T) or ACCA or equivalent qualification and registered with NBAA; and a Master Degrees in Business Administration I Finance/Planning or related qualifications. WORKING EXPERIENCE REQUIRED At least eight (8) years of working experience in public or any reputable private organization three (3) of which must be in a Seni

Msajili wa Vyama vya Siasa AIGOMEA Barua ya Maalim Seif ya Kuwavua Uanachama Wabunge wa CUF

Image
Mgogogoro ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unaendelea kufukuta baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jon Ndugai akimtaarifu kuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limewasimamisha uanachama wanachama wawili wa chama hicho ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua) na Maftaha Nachuma (Mbunge wa Mtwara Mjini) uamuzi uliofikiwa kutokana na wajumbe wa mkutano huo kupiga kura za siri na kuamua kuwavua uanachama, hivyo kumuomba Spika Ndugai afanye utaratibu wa kuwavua ubunge wao kwa kuwa si wanachama halali wa chama hicho. Baada ya barua hiyo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amejibu barua ya Maalim Seif kwa kuwa kueleza kutomtambua yeye kama Katibu Mkuu wa CUF kwakuwa barua kutoka chama hicho ilisema kuwa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama inakaimiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haijapokea barua nyingine ku

MREMBO AGNESS MASOGANGE YAMKUTA YA WEMA

Image
Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali amesema mkojo wa mrembo Agness Gerald 'Masogange' umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroine na oxazepam (Diacety Imophine). Mkemia Elias Mulima (40) ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kwamba sampuli ya mkojo wa Agness zilizowasilishwa kwao zilikua na chembechembe za dawa za kulevya. Mulima ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya Masogange kukutwa na dawa za kulevya Februari 15, 2017 Dar es salaam akiongozwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula, Shahidi huyo amedai kuwa Februari 15 mwaka huu katika ofisi ya Mkemia mkuu Dar es salaam akiwa ofisini alipokea vielelezo kutoka Jeshi la Polisi vilivyowasilishwa na koplo Sospeter na WP Judith kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni dawa za kulevya au la. Pia shahidi huyo ameongeza kwa kudai kuwa iliwasilishwa na fomu maalumu ya dawa za kulevya ambayo ilikua na namba DCEA 008 na alifanya usajil

Mbunge Haonga wa Chadema Akamatwa kwa Madai ya Uchochezi

Image
Muendelezo wa wabunge wa upinzani kutiwa nguvuni kwa tuhuma mbalimbali umezidi kushika kasi baada ya leo Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe, Pascal Haonga, kukamatwa na Polisi leo mchana akiwa katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi. Mbunge huyo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kufanya mkusanyiko usio halali. Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, kuthibitisha kumshikilia Haonga lakini hakutaka kueleza suala hilo kwa kina kwa madai kuwa hayupo ofisini. Meshack Mgaya ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Songwe amesema kuwa chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu kukamatwa kwa kada huyo na kwamba baada ya kujiridhisha watato tamko