MREMBO AGNESS MASOGANGE YAMKUTA YA WEMA
Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali amesema mkojo wa mrembo Agness Gerald 'Masogange' umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroine na oxazepam (Diacety Imophine).
Mkemia Elias Mulima (40) ameiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri kwamba sampuli ya mkojo wa Agness zilizowasilishwa kwao
zilikua na chembechembe za dawa za kulevya.
Mulima ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya Masogange kukutwa na
dawa za kulevya Februari 15, 2017 Dar es salaam akiongozwa na Wakili wa
Serikali Constantine Kakula, Shahidi huyo amedai kuwa Februari 15 mwaka
huu katika ofisi ya Mkemia mkuu Dar es salaam akiwa ofisini alipokea
vielelezo kutoka Jeshi la Polisi vilivyowasilishwa na koplo Sospeter na
WP Judith kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni dawa za
kulevya au la.
Pia shahidi huyo ameongeza kwa kudai kuwa iliwasilishwa na fomu maalumu
ya dawa za kulevya ambayo ilikua na namba DCEA 008 na alifanya usajili
na kuipa namba ya maabara 446/2017 ambapo Mshtakiwa alipewa kontena
maalumu kwa ajili ya sampuli ya mkojo.
Pamoja na hayo Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alipinga kupokelewa kwa
kielelezo hicho kwa sababu Polisi walitakiwa kuiomba Mahakama ili
wachukue vipimo vya Mshitakiwa lakini hawakufanya hivyo na kudai ni
kinyume na sheria 63 CPA.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi
Agosti 28/2017 ambapo siku hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kupokea ama
kutopokea vielelezo vya sampuli ya mkojo wa Agnes Masogange kutoka
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Comments
Post a Comment