MARUBANI WAKIONA CHA MOTO BAADA YA KUMRUHUSU MTOTO KURUSHA NDEGE
Serikali
nchini Algeria, imewafukuzwa kazi marubani wawili wanaofanya kazi
katika shirika la ndege la serikali baada ya kumruhusu mtoto wa miaka 10
kuendesha ndege.
Mtoto
huyo anayedaiwa kuwa ni yatima alikuwa akiendesha ndege aina ya Air
Algerie, iliokuwa na abiria ndani na ilifanya safari zake katika mji wa
Algiers hadi Setif.
Zoezi
la mtoto huyo kuendesha ndege lilifadhiliwa na kurekodiwa kituo cha El
Bilad TV, ambapo walionyesha tukio zima huku kijana huyo akiwa amevalia
sare za rubani.
Baada
ya video na picha kusambaa za kijana huyo akiongoza ndege, ndipo
serikali ilichukua hatua ya kuwafukuzwa kazi Marubani hao mnamo Julai 29
mwaka huu.
Comments
Post a Comment