Polisi limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu kwa wafanyabiashara wa TV, Simu na Computer “USED”
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Kaimu Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dsm Lucas Mkondya amesema katika miezi ya hivi karibu kumeibuka wizi wa Uvunjaji majumbani ambao wahalifu huchuku Tv hasa zile Flat screen ambapo jeshi hilo limebaini hupelekwa katika maduka hayo.
Jeshi hilo pia litawakamata watu wote wanaoendesha biashara ya magari yasiokuwa katika yard katika maeneo ya jiji la Dsm.
Aidha jeshi hilo pia kuanzia jumatatu litaendesha Msako wa Kukamata magari yote yenye Vioo vyeusi maarufu TINTED baada ya kubaini kuwa baadhi ya wahusika hujihusisha na Uhalifu na Uporaji,kuficha mali za wizi lakini pia kufanyia vitendo visivyofaa vya Uzinzi.
Akizungumzia matukio ya Uhalifu amesema watu wawili wanaosadikiwa ni majambazi wakiwa katika pikipiki eneo la upanga walimvamia na kupora kiasi cha milion 10 raia wa kihindi ambapo katika purukushani jambazi mmoja alikimbia huku aliyekuwa na bastora alidhibitiwa na kuuwawa na wananchi.
Aidha katika kutekeleza agizo la jeshi la polisi kwa majambazi waliohukumiwa na kutoka jela kujisalimisha polisi ili kujua shughuli zao,majambazi 24 wamejisalimisha huku 14 wametakiwa kujisalimisha au kusakwa na jeshi hilo.
Comments
Post a Comment