MARUBANI WAKIONA CHA MOTO BAADA YA KUMRUHUSU MTOTO KURUSHA NDEGE
Serikali nchini Algeria, imewafukuzwa kazi marubani wawili wanaofanya kazi katika shirika la ndege la serikali baada ya kumruhusu mtoto wa miaka 10 kuendesha ndege. Mtoto huyo anayedaiwa kuwa ni yatima alikuwa akiendesha ndege aina ya Air Algerie, iliokuwa na abiria ndani na ilifanya safari zake katika mji wa Algiers hadi Setif. Zoezi la mtoto huyo kuendesha ndege lilifadhiliwa na kurekodiwa kituo cha El Bilad TV, ambapo walionyesha tukio zima huku kijana huyo akiwa amevalia sare za rubani. Baada ya video na picha kusambaa za kijana huyo akiongoza ndege, ndipo serikali ilichukua hatua ya kuwafukuzwa kazi Marubani hao mnamo Julai 29 mwaka huu.