CHADEMA Yalia na Ugumu wa Maisha kwa Wananchi
Mbowe amesema mwakà 2015, NFRA ilihifadhi tani 446,000 za chakula lakini kufikia mwaka huu wakala huyo amehifadhi tani 74,826 za chakula.
Mbowe amesema chakula kinapanda bei kwa sababu hakuna mkakati wowote wa Serikali kuwainua wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo.
"Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna usalama wa Taifa.
"Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka
"Bei ya mahindi kwa mwakà 2015 ilikuwa ndogo lakini mwaka huu imefika zaidi ya 90,000. Wananchi wanapata shida kwa sababu Serikali yao imewatupa wakulima." Amesema Mbowe
Comments
Post a Comment