MAJADILIANO SERIKALI NA BARRICK GOLD YAANZA RASMI

Waziri
wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais. John Magufuli
kujadiliana na uongozi wa Barrick Gold Corporation akiwa na ujumbe wa
kampuni hiyo kabla ya kuanza mazungumzo hayo leo jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Majadiliano
kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi
kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu madini yanayochimbwa
na kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam.
Prof. Kabudi akiwaelekeza jambo.
Taarifa
ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, imesema
kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa
Palamagamba Kabudi na kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa
Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams.
Prof. Kabudi akiwa na wageni hao.
Profesa
Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri
kujadiliana na Barrick juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya
madini ya kampuni hiyo nchini na itahakikisha inasimamia masilahi ya
nchi ipasavyo.
Prof. Kabudi akipata picha ya pamoja na ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo.
Imeelezwa
Williams ameshukuru uwepo wa majadiliano hayo akisema Barrick imepokea
madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na
kufikia makubaliano yenye masilahi kwa pande zote mbili.
Prof.
Kabudi akizungumza akiwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni hiyo,
Richard Williams, kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo.
Rais
aliunda kamati hiyo baada ya kupokea ripoti za kamati zingine mbili,
moja ilichunguza mchanga wa madini (makinikia) na nyingine ya kitaalamu
iliyochunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga huo
unaosafirishwa nje ya nchi.
Comments
Post a Comment