IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI CHA UBUNGO
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ( katika) akiwa katika ukaguzi
wa kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani
cha Ubungo, (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamanda wa Kanda maalum ya Dar
es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP) Lucas Mkondya akifuatiwa na
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam,
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Haji.
Na Jeshi la Polisi
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka madereva na wamiliki
wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na wamiliki
na madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala kuhakikisha
wanayafanyia ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili
kupunguza ajali zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa magari.
IGP Sirro
aliyasema hayo jana wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika
Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na kituo
cha daladala cha Mbezi Luisi kwa lengo la kuangalia hali ya usalama wa
kituo hicho, kuona namna ukaguzi wa mabasi ya abiria unavyofanyika kabla
hayajaanza pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za abiria.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (katika) alipofanya ukaguzi wa
kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha
Ubungo na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi, (kushoto) ni Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Murilo
Jumanne Murilo. Nimefarijika kuona watendaji wa kituo hiki pamoja na
askari wangu wakifanya kazi vizuri kwa ushirikiano mkubwa hali
inayosaidia kupunguza kero mbalimbali kwa watumiaji wa kituo hiki”
alisema IGP Sirro.Aliongeza kuwa Ubungo ni salama na itaendelea kuwa
salama kwa sababu vibaka wamepungua na wale wanaofanya utapeli katika
kituo hicho waache mara moja na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa mwisho
wa siku wataacha familia zao baada ya kukumbana na mkono wa sheria.Pia
ameelekeza magari yote ya abiria yabandikwe namba simu zote za makamanda
wa mikoa wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Wakuu wa Polisi wa
wilaya zote sehemu ambazo itakuwa ni rahisi kuonekana na abiria ili iwe
rahisi kwao kutoa taarifa pindi wanapoona dereva anaendesha gari kwa
kukiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Aliwataka
wananchi kuendelae kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa
za uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti na
kutoa wito kwa wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kuwa
wastaabu na kuhakikisha wanaheshimu sheria na kanuni za usalama
barabarani kwa kuwa kila mmoja anafahamu madhara ya ajali.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na madereva wa
mabasi ya abiria pamoja na abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda mikoa
mbalimbali na nchi jirani baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika
Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo,
pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luis.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimuelekeza Kamanda wa Kikosi
cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Fortunatus Muslim kuhakikisha kuwa magari na mabasi yote ya abiria
yanakaguliwa mara kwa mara. IGP Sirro alifanya ukaguzi wa kushtukiza
jana katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha
Ubungo na Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis.
Comments
Post a Comment