IGP SIRRO ALIPONGEZA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipiga saluti wakati wa paredi
ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua mapema
leo kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa
jeshi la polisi mjini Singida leo piga saluti wakati wa paredi ya
polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa
habari muda mfupi baada kukagua askari polisi waliokuwa kwenye paredi
kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa.
………………………….
Picha/Habari na Gasper Andrew.
Mkuu wa
Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amelipongeza jeshi la polisi
Mkoani Singida kwa juhudi zake za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo
ya utekeji wa magari kwa kiwango kikumbwa.IGP Siro ametoa pongezi hizo
leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kweye viwanja
vya kambi ya kikosi cha kuzuia fujo (FFU) mjini hapa.Amesema matukio
ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa
kwa sasa, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.“Hatua hii inachangia
uwepo wa amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa wa Singida hivyo
kutoa fursa kuweza kujiletea maendeleo yao ya mkoa na taifa kwa
ujumla” amesema.
IGP Siro
amesema mafanikio hayo yamechangiwa na wananchi kwa kiwanngo
kikubwa kwa kutoa ushuirikiano kwa jeshi la polisi. Akifafanua amesema
wananchi wamekuwa wakitoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa jeshi la
polisi pindi wanapobaini dalili ama matukio ya kihalifu.“Kwa sasa
kwa kweli wananchi hata ninyi waandishi wa habari mnatupa ushirikiano
mzuri sana. Ushirikiano huu unachangia kazi zetu kuwa nyepesi na za
mafanikio makubwa. Sasa hivi kule Kibiti mkoani Pwani, wananchi
wanatusaidia mno taarifa zinazohusu mauaji ya watu wasiokuwa na
hatia”, amefafanua zaidi.IGP Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa
wivu na nchi jirani kwa namna tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na
kupelekea nchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Wakati
huo huo, Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo kuwaomba
wananchi waendelee kushirikiana na jeshi hilo, kufichua baadhi ya
watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu ili waweze
kuchukulia hatua stahiki.
Comments
Post a Comment