WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AMVAA TUNDU LISSU,AFUNGUKA LIVE
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ‘amemvaa’ Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwamba amejaribu kutengeneza kila aina ya kichaka kukwamisha jitihada za Rais John Magufuli kupambana na usafirishaji holela wa madini nje ya nchi bila mafanikio. Ingawa Mwigulu hakumtaja jina Lissu moja kwa moja alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Zinzirigi kilichopo katika Jimbo lake la Iramba Magharibi pia mkoani Singida juzi, hoja nyingi alizogusia ni zile ambazo Lissu amekuwa akinukuliwa kuzisema. Moja ya hoja hizo ni ile ambayo Mwigulu alisema watu wenye nia mbaya walianza kusema kuwa Serikali itashtakiwa kwa hatua yake ya kuzuia makontena 277 ya mchanga wenye dhahabu. “Baadaye watu haohao walisema tena kwamba mchanga ule ni takataka tu lakini walipoambiwa wasisafirishe mchanga huo wenye madini walisema wanapata hasara ya Sh4 trilioni kwa siku.” Hata hivyo, Acacia walisema wanapata hasara ya dola bilioni moja kila siku. Pia, Mwigulu alise