Ishu ya Mchele wa Plastiki Bongo, Kiwanda Kinachodaiwa Kutengeneza Chavamiwa



DAR ES SALAAM: Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi una­osambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, juu ya kuwepo kwa mchele wa plastiki, unaodaiwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu, unaouzwa katika vibanda vya akina mama n’tilie.
 Kinu chenye malighafi ya kutengeneza plastiki hizo.

Baada ya uvumi huo kuleta hofu kubwa kwa wananchi, hasa kufuatia video mitandaoni kuonyesha wali uli­opikwa ukiliwa na hata kiwanda kina­chodaiwa kuwepo nchini kinachoten­geneza mchele huo, Risasi Jumamosi liliamua kuufanyia kazi uvumi huo ili kujua mbivu na mbichi ya sakata hilo.

Malighafi zinazotumika kutengeneza plastiki hizo hapo kiwandani.

Risasi Jumamosi liliambiwa kuwa mchele huo unauzwa katika baadhi ya masoko ya jijini Dar es Salaam yakita­jwa kuwa ni pamoja na yale ya Bugu­runi, Mwananyamala, Makumbusho na Afrikasana.
Kikosi kazi kilisambazwa katika masoko hayo na kufanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuzungumza na baadhi ya wanaouza bidhaa hiyo.

Mifuko yenye plastiki ndani yake ikikaguliwa

Lucas Kimadi wa Soko la Makum­busho anasema; “Hata hivyo, ingawa nimesikia juu ya tetesi hizo kiuk­weli sijawahi kuuona machoni mchele huo wa plastiki. Ila nime­wahi kusikia siku za nyuma kuwa kuna wafanyabiashara walikuwa wanauingiza kinyemela na seri­kali iliwachukulia hatua.”

Bango la kiwanda hicho lililoandikwa Kalunde Mill.

Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwesigwa, alipoulizwa juu ya ku­wepo kwa mchele huo, alisema anavyofahamu, hayo ni maneno ya mitandaoni, kwani hajawahi kuuona.

“Sasa kama ni wa plastiki utaupikaje na uwe tayari kwa kula. Watu wameamua kuvumi­sha tu lakini sidhani kama kuna ukweli katika hili, na ninakubal­iana kabisa na TFDA pengine hiyo video ambayo tumeiona mtandaoni inaonesha namna ya kutengeneza mifuko.”

Mmiliki wa kiwanda hicho Mika (kulia) akihojiwa.

Hali kama hiyo ilikuwepo pia katika masoko yote ambako Risa­si Jumamosi lilitembelea, kwani wafanyabiashara wote walionye­sha kushangazwa kwao na madai hayo, wakisema hivi sasa baada ya mavuno, wanapata mchele mwingi kutoka Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Morogoro na Mwanza na kwamba siyo rahisi kwao kuuza wala kununua mchele wa plastiki.

Polisi wakikagua usajili wa kiwanda hicho.

 “Mimi kiukweli nimewahi kusi­kia hata hapahapa kwamba kuna watu walikuwa wanauuza mchele huo kinyemela, lakini sijawahi ku­waona kwa macho wala kuuona mchele wenyewe.
“Nahisi hayo ni maneno ya mitandaoni, nimekuwa nikisikia mara kwa mara watu wanasema juu ya hilo lakini sijawahi ka­bisa kupata mtu wa kunithibit­ishia kuwa mchele wenyewe huu hapa,” alisema Rajabu Simba wa Soko la Mwananyamala.

Mkaguzi wa Polisi akikagua kiwanda hicho.

“Nimeona kwenye mitandao kuwa mchele huo upo lakini si­jawahi kuuona, kununua wala kushawishiwa kuuziwa ili nije ni­fanye biashara.”
Naye katibu wa soko hilo, Fu­rahisha Kambi alisema sokoni hapo hakujawahi kutokea tetesi za kuwepo kwa mchele wa plastiki ingawa amewahi kuzisikia mara kadhaa huko nyuma.



Wakati kikosi kazi hicho kikiwa kazini, mara zikaibuka taarifa za kiintelijensia, zikisema kuwa askari polisi walikuwa wakijiandaa kwen­da kuvamia kiwanda kimoja huko Kiwalani Minazi Mirefu, kinachod­haniwa kuwa ndicho kinachozalisha mchele huo wa plastiki.
Mara moja, kikosi hicho kilijigawa na kufanikiwa kujiunga na wanaus­alama hao, ambao kwa wakati huo walikuwa wakiandaa hati maalum ya upekuzi (Search Warrant).

Mifuko ya plastiki baada ya iliyotengenezwa kiwandani hapo.

Msafara wa watu hao wa usalama uliwasili eneo la tukio wakiwa chini ya ofisa mmoja ambaye alikataa jina lake kuandikwa gazetini na kuikuta nyumba inayotumika kama kiwan­da, mbele ikionyesha kuwa ni duka la unga, mchele kwa bei ya jumla.
Ndani ya kiwanda hicho, kili­chokuwa na wafanyakazi wachache wa kiume na kike, Risasi Jumamosi lilishuhudia mashine zikiunguruma huku rola za plastiki zikizunguka na kuishia kwenye kitu kama ndoo ambapo punje za kitu kama mchele zilionekana kudondokea.

Rola zinazotengeneza mifuko ndani ya kiwanda hicho.

Risasi Jumamosi lilishuhudia pun­je hizo na kuzishika zikifanana kwa kiasi kikubwa na zile za mchele, la­kini mmiliki wa kiwanda hicho, aliye­jitambulisha kwa jina moja la Mika, alisema kinachoonekana kama mchele, ni ‘matirio’ ya kutengeneza plastiki.

“Hapana mwandishi, huo siyo mchele, hayo ni matirio ya plastiki ambayo ndiyo tunatengenezea hii mifuko unayoiona.”

Alipoulizwa kwa nini nje ya kiwan­da, kumeandikwa kama kunauzwa mchele na unga badala ya mifuko ya plastiki, alisema awali kiwanda hicho kilitumika kama duka la jumla la bidhaa hizo na yeye hakuwa ame­futa tangazo hilo.

Rola zinazotengeneza mifuko.

“Aaaa unajua hili jengo hapo awali lilikuwa likitumika kama mashine ya kusaga na kuuza huo unga na mchele, alivyohama mimi ndiyo nikalichukua na kuendeshea hii bi­ashara yangu ya kuzalisha mifuko ya plasti.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa akifanya ukaguzi kwenye kiwanda hicho.

Maofisa wa Polisi waliokuwemo katika msafara huo, baada ya kufan­ya naye mahojiano ya kina na kujiri­dhisha jinsi utengenezaji wa mifuko hiyo ya plastiki ulivyo, walimuachia mmiliki huyo.
Wakati tayari Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ikiwa imetoa tan­gazo la kupinga kuwepo kwa bid­haa hiyo sokoni, Risasi Jumamosi linaweza kuripoti kwa sasa kuwa uvumi juu ya kuwepo kwa mchele wa plastiki sokoni ni uongo, un­aoenezwa na watu wenye malengo wanayojua wenyewe.

Wafanyakazi ndani ya kiwanda hicho.

Hata hivyo, bado linaendelea ku­fuatilia kwa karibu tetesi hizo na litatoa taarifa nyingine haraka kwa wasomaji na vyombo vinavyohusi­ka endapo litabaini kuwepo kwake, sambamba na wote wanaoeneza taarifa hizo zenye kuwatia hofu wa­nanchi.

Folonya zikiwa zimejaa mifuko ya plastiki.

Yusuf Miraji wa Afrikasana al­isema amefanya biashara hiyo kwa muda mrefu, lakini hajawahi kuuona mchele wa plastiki. Alidai huenda watu wanachanganya ule wa Basmati, wakidhani ndiyo wa plastiki.
 Lango la kuingia kiwandani humo.

Katika Soko la Buguruni, Risasi Jumamosi lilifanikiwa kuzungum­za na Halima Msuye, muuzaji wa mchele wa muda mrefu katika soko hilo ambaye alisema;

STORI: WAANDISHI WETU | RISASI JUMAMOSI

Comments

Popular posts from this blog