KIJANA AJINYONGA JUU YA MTI KWA UGUMU WA MAISHA
Matukio
ya watu kuchukua maamuzi ya kujiua katika manispaa ya Shinyanga yanazidi
kushika kasi ambapo jana Jumapili June 18,2017 majira ya saa 10
alfajiri kijana aitwaye Paulo Ezekiel (17) mkazi wa mtaa wa Mazinge kata
ya Ndembezi alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti jirani
na nyumba yao.Inaelezwa kuwa huenda ni ugumu wa maisha ndiyo umechangia
kifo cha kijana huyo kwani enzi za uhai wake alikuwa analalamika kuwa
maisha ni magumu.
Baba
mzazi wa marehemu Ezekiel Paulo anasema majira ya saa 10 alisikia mlango
wa chumba cha kijana wake ukifunguliwa akadhani pengine ametoka kwenda
kujisaidia lakini hakurudi tena ndipo alipoingiwa na wasiwasi na kuanza
kumsaka.“Tuliamshana tukaanza kumsaka kila mahali baadaye tukamuona
akiwa juu ya mti jirani na nyumba yetu tayari amefariki dunia”, ameeleza
Paulo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa tukio.
Matukio
ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua yameanza kukithiri katika manispaa ya
Shinyanga ambapo ndani ya mwezi mmoja huu wa Juni hili ni tukio la nne.
Tukio la
kwanza ni la Luhende Lusangija (34) mkazi wa kata ya Ngokolo aliyejiua
kwa kamba,la pili ni la Mwenyekiti wa waendesha bodaboda katika manispaa
ya Shinyanga Jacob Paul mkazi wa kata ya Ngokolo aliyejiua kwa waya wa
simu la tatu ni la Saada Elias mkazi wa kata ya Ndembezi aliyekatisha
maisha yake kwa kujichinja kwa kisu na chupa ya soda.
Comments
Post a Comment