MSANII ESTER APANGIWA MJENGO NA MWANAUME
MSANII wa
filamu za Kibongo, Ester Kiama anadaiwa kupangishiwa mjengo na mwanaume
ambaye ni mume wa mtu aliyemhamisha kutoka Kijitonyama alikokuwa
anaishi na kumwamishia Mbezi Beach.
Chanzo
makini kilieleza kuwa kwa sasa Ester anaishi kwenye nyumba nzima yenye
hadhi tofauti na alikokuwa akiishi mwanzo ambapo amelipiwa kodi ya mwaka
mzima na mwanaume huyo.
Risasi Jumamosi lilimtafuta
Ester ili kujibu tuhuma hizo na alipopatikana alikiri kuhamia Mbezi
Beach kwenye nyumba nyingine nzima lakini alipinga suala la
kupangishiwa na mwanaume.
“Ninaishi
Mbezi Beach kwa sasa ambako nimehamia hivi karibuni, habari za kwamba
nimelipiwa kodi na mwanaume ni uongo, nimejilipia mwenyewe,” alisema
Ester.
Comments
Post a Comment