Undani wa Kifo Cha Mume wa Zari Nyuma ya Pazia
Staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, akiwa na aliyekuwa mume wake Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ enzi za uhai wake. STORI: SIFAEL PAUL, RISASI JUMAMOSI, MTANDAO KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia. Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi. Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’ alipokuwa hospitali. MARA YA MWISHO KUONEKANA Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pat