Dalili za Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo
Hapo
kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo, kisha tukasoma
kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo, tukasoma tena kuhusu chakula
cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na leo tunaendelea kuangalia dalili za
ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na;
Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na;
- Kuchoka choka sana bila sababu maalum
- Kuuma mgongo au kiuno
- Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
- Kizunguzungu
- Kukosa usingizi
- Usingizi wa mara kwa mara
- Maumivu makali sehemu ya mwili
- Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
- Kichefuchefu
- Kiungulia
- Tumbo kujaa gesi
- Tumbo kuwaka moto
- Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
- Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
- Kutapika nyongo
- Kutapika damu au kuharisha
- Sehemu za mwili kupata ganzi
- Kukosa hamu ya kula
- Kula kupita kiasi
- Kusahahu sahau na
- Hasira bila sababu.
Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
Comments
Post a Comment