NAIBU WAZIRI DKT.KINGWANGALLA AMTEMBELEA MZEE MAIGE’NGOSHA ‘ MUHIMBILI

Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kingwangalla akiongea na Mzee Maige ambaye amelazwa kwenye chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo asubuhi ya leo mzee huyo alihamishiwa hapo kwa uchunguzi wa afya na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura Renatus Tarimo(kushoto) akimueleza Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto jinsi walivyompokea na kumuhudumia kwenye kitengo chao na hali ilivyo hadi sasa,Dkt. Tarimo amesema hali ya Mzee maige inaendelea vizuri na wameshamfanyia uchunguzi wa awali na wanaendelea na uchunguzi zaidi

Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga (katikati) akimueleza jambo Naibu Waziri Dkt. Kingwangalla mara baada ya kutoka kwenye chumba alicholazwa Mzee Maige.Mzee Maige au kwa jina maarufu anajulikana kama Ngosha ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa ambayo inatumika hadi sasa nchini.


Naibu Waziri Dkt.Kingwangalla akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt.Mfinanga(kulia) mara baada ya kumjulia hali Mzee aliyebuni nembo ya Taifa Mzee Francis Maige kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Hospitali hiyo,kushoto ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Profesa Laurence Maseru

Mzee Maige akiongea na Naibu Waziri,Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Kingwangalla(Picha na Catherine Sungura-WAMJW)

Comments

Popular posts from this blog