TABIA 4 ZINAZOHARIBU KINGA ZA MWILI BILA KUJIJUA
Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali. Mtu
anapokuwa na kinga imara za mwili, huepuka kuugua mara kwa mara na kwa
kifupi unaweza kusema kwamba kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika afya
ya binadamu. Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na hivyo unahitaji kuchukua hatua za kuziimarisha.Kwa
kawaida Mungu alituumba miili yetu ikiwa na uwezo wa kujikinga na
magonjwa yote, laikini mwili utaweza kufanya hivyo endapo tu utapatiwa
vyakula vinavyohitaji ili kuimarisha kinga zake.
Leo tuangalia aina ya vyakula vya kuepuka ili kuzifanya kinga za mwili kufanya kazi zake vizuri.
1. Mhusika anapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi
Sukari
siyo nzuri kwa afya yetu hasa inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha
kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo
(teaspoon), kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga
ya mwili. Inaelezwa kuwa chupa moja ya soda ina karibu vijiko 6 vya
sukari. Hivyo kama wewe ni mnywaji mkubwa wa soda na vinywaji vingine
vya aina hiyo, utaona ni kiasi gani unachangia kuharibu kinga zako za
mwili.
2. Epuka unywaji wa vileo
Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sumu ndani ya miili yetu. hivyo si nzuri pia kwani huweza kuchangia kudhoofisha kinga za mwili.
3. Epuka matumizi ya vyakula vya kukaanga
Vyakula
vya kukaanga kama vile chips na vinginevyo, pamoja na vyakula vya kuoka
huwa na mafuta mabaya ambayo huwa na tabia ya kutengeneza magonjwa
mwilini (fee radicals) ambayo huathiri mfumo wa kinga ya mwili pamoja na
chembechembe za nasaba (DNA). Vyakula hivi vinapaswa kuliwa kwa nadra
sana au kuepukwa kabisa ikiwezekana.
4. Epuka vyakula vya viwandani (vyakula vya makopo)
Epuka
ulaji wa vyakula vya kwenye makopo na badala yake pendelea kula vyakula
halisi‘fresh’ na vya asili. Ulaji wa vyakula vya asili, hasa vyakula
vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, huwa na idadi kubwa ya vitamini,
madini na kamba-lishe ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha mfumo wa
kinga ya mwili.
Comments
Post a Comment