Faida (6) za tangawizi

Siku kadhaa zilizopita tuliona kwa uchache faida za tangawizi, naomba siku ya leo tuendelee faida nyingine za tangawizi ambazo ni;

1. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo
Wataalamu wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye ubongo bila shida.

2. Huondoa gesi tumboni
Tangawizi husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi yanayosababishwa na ulaji.

3. Husaidia kutibu mafua, kikohozi
Unachitakiwa kufanya. Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi.

4. Huongeza nguvu za kiume
Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo.

5.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao.
Kwa kina mama wanaonyenyesha tangawizi inachochea ongezeko la maziwa, hivyo hufanya mama kuwa na maziwa mengi ya kumtosha mtoto. Hata kwa kina mama wenye tatizo la uhaba wa maziwa, pia ni vizuri kutumia tangawizi kama kinywaji cha moto, kama Chai.

6.husaidia kuondoa kichefuchefu.
Kwa kina mama wajawazito, wanopata kichefuchefu na kutapika inasaidia sana kuondoa hali hiyo.

Unachotakiwa kufanya. Tafuna kipande cha tangawizi badala ya ndimu.

Comments

Popular posts from this blog