Dodoma waanza kutenga maeneo ya biashara


MWENYEKITI wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ambaye pia ni Diwani wa Kikuyu Kusini, Anselm Kutika amesema kata zote za Manispaa za Dodoma zitatenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara, jambo litakaloondoa tatizo la wafanyabiashara kufanya kazi zao katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Kutika alisema kata zote za Manispaa ya Dodoma ni lazima zitenge maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ili kuuweka mji katika hali ya usafi. Alitaja sehemu ambazo tayari zimetenga maeneo kwa ajili ya biashara kuwa ni Kisasa, Tambukareli, Kikuyu Kusini, Kizota, Chang’ombe, Nkuhungu, Makole na Kiwanja cha Ndege.

“Kamati ya Mipango Miji imepitipisha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara na maeneo hayo yatakuwa kikata na wananchi watakuwa walinzi namba moja,” alisema. Akaongeza, “Kikuyu Kusini tulitoa matangazo kama kuna mtu aliyefikiwa na tangazo na walengwa walikuwa ni wakazi wa kata, hapo awali changamoto ilikuwa baadhi ya D centre zilivamiwa na wakazi wan je ya kata.”

Alisema baadhi ya stendi zilizokuwa katikati ya mji zimeenda nje ya mji na kumekuwa na nafuu kwani msongamano umepungua. Kutika aliwataka wafanyabiashara kufuata taratibu wanapopata maeneo ya kufanyia biashara kwa kubaki huko na si kurudi mitaani na kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Comments

Popular posts from this blog