Posts

Breaking Nwez: Simba Yabaki Na Pointi Tatu Ilizopewa Na Kamati Ya Saa 72

Image
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemaliza kikao chake na Simba inaendelea kubaki na pointi ilizopewa na Kagera Sugar. Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine, amesema kamati hiyo itakaa tena na kuna shahidi wengine wataitwa kuhojiwa. Kikao hicho kimefanyika kuanzia leo asubuhi  katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na waamuzi, wafanyakazi wa bodi ya ligi, viongozi wa simba, Kagera Sugar, waamuzi wa mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya African Lyon na beki Mohammed Fakhi wamehojiwa. Baada ya kuhojiwa, kilichofuatia lilikuwa ni suala la kamati kukaa kwa takribani saa moja kuonyesha walikuwa wakimalizia kuhusiana na kile walichowahoji wahusika. Kabla, kamati ya Saa 72, ilikuwa imeipa Simba pointi tatu na mabao matatu licha ya kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar. Kamati ya Saa 72, ilibaini Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akiwa na kadi tatu za njan

Wema Sepetu arudi kwa kasi bongo movie

Image
Tanzanian SweetieHeart Wema Sepetu amewataka watanzania ukaa mkao wa kula kwa kazi yake mpya Hii ni kufuata mfukulizo wa post zake kuhusu ujio wake mpya wa kazi zake katika kuigiza, amewaasa wabongo kuwapa ushirikiano wa dhati kabisa kwani amedhamiria kuirudisha Bongo Movies katika kiwango cha enzi zile za Kanumba Tanzanian SweetieHeart Wema Sepetu amewataka watanzania ukaa mkao wa kula kwa kazi yake mpya Hii ni kufuata mfukulizo wa post zake kuhusu ujio wake mpya wa kazi zake katika kuigiza, amewaasa wabongo kuwapa ushirikiano wa dhati kabisa kwani amedhamiria kuirudisha Bongo Movies katika kiwango cha enzi zile za Kanumba

Njia ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda/ Kuzuia Mimba Kwa Njia ya Kalenda

Image
Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke. Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii, kwa hiyo pamoja na kutoa maelezo ya jinsi ya kutumia, sisi hatumshauri mtu kutumia njia hiyo.  Nani anaweza kutumia njia ya kalenda Moja,  Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo. Pili,  Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Tatu, Wanawake wanaojua hisabati vizuri sana.  Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii i

Kikosi hatari cha US NAVY 'SEAL' chatua rasmi Korea Kasikazini

Image
NI wazi kuwa jaribio lilifanywa na Korea Kaskazini la Makombora yake ya Nukria  limeshtua  Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani. Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani. Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land. Ni Mara chache s

VIONGOZI WA DINI WAJUMUIKA KUFANYA DUA MAALUM KUZIOMBEA MKURANGA NA KIBITI

Image
Rufiji. Viongozi wa dini ya Kiislamu Mkoa wa Pwani, wamefanya dua maalumu ya kuuombea mkoa huo ili kuirejesha hali ya usalama. Dua hiyo imefanywa wakati wilaya tatu za mkoa huo, Kibiti, Mkuranga na Rufiji zikikabiliwa na matukio ya mauaji ya mara kwa mara ya wenyeviti wa vijiji na maaskari polisi Alhamisi iliyopita watu wasiofahamika waliwashambulia na kuwaua polisi wanane waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu, wilayani Kibiti. Askari mmoja alinusurika na kujeruhiwa mkononi. Mauaji mengine yanayotokea katika maeneo hayo ni kama lile la kuuawa kwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya. Hadi sasa viongozi wa vijiji zaidi ya 10, katika wilaya hizo wameuawa kwa kupigwa risasi au kukatwa mapanga tangu mwaka jana. Wakizungumza katika dua hiyo iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa, Ikwiriri juzi, Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Wilaya ya Mkuranga Sheikh Mohammed Katundu alisema wao kama viongozi wa dini wamelazimika kufanya ibada hi

Ufisadi Mkubwa Wizara ya Afya Wagundulika..Wakati Watoto Wakikosa Chanjo Mahospitalini..Hivi Ndivyo Mabilioni ya Pesa Yalivyotafunwa na Wajanja Wachache..!!!

Image
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha 2015/16 imebaini ufisadi wa mabilioni ya fedha katika mradi wa chanjo ya Surua Rubella na ameshauri kufanyika uchunguzi wa kijinai na waliohusika warejeshe fedha hizo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hayo yalibainika wakati wa ukaguzi maalumu katika halmashauri za wilaya na ofisi za waganga wakuu wa mikoa. Ukaguzi huo umebaini Sh20.9 bilioni zilipokelewa na Wizara ya Fedha kutoka Gavi Alliance na kiwango hicho chote kilipelekwa Wizara ya Afya kugharamia chanjo ya Surua Rubella. Kati ya kiwango hicho, Sh19.09 bilioni zilitolewa kwa ajili ya chanjo; Sh18.3 bilioni zilitumika Tanzania Bara na Sh725 milioni zilipelekwa Zanzibar na Sh1 bilioni zilitumika kama gharama za uendeshaji. Ripoti hiyo imeainisha kuwa hadi Desemba 31, 2014 kulikuwa na bakaa ya Sh838,423,408. Fedha zilizopokelewa halmashauri Ripoti hiyo inaainisha kuwa Sh17.3 bilioni zilitumwa katika mikoa na kuing

Kwa Mara Nyingine Tena Mke wa Rom Amefunguka Haya Makubwa Kuhusu Tukio la Kutekwa kwa Mumewake Roma Mkatoliki..!!!

Image
Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu. Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo. “(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki. Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu. “Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy. Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na mati

Huyu Hapa Muuza Madawa ya Kulevya Aliyependwa na Wananchi Mpaka Kupewa Jina la Yesu na Mlinzi wa Amani

Image
TAJIRI WA UNGA AKAWA MWEMA MPAKA AKAITWA YESU Christopher Coke a.k.a Dudus, ni tajiri wa dawa za kulevya, akiongoza genge la Shower Posse. Genge hilo na mtandao mzima wa unga, Dudus au President alirithi kutoka kwa baba yake, Lester Coke a.k.a Jim Brown au Ba-Bye aliyeuawa gerezani mwaka 1992. Shower Posse makao makuu yake yapo Tivoli Gardens, Kingston, Jamaica. Dudu alikuwa mtu mwema. Alisaidia fedha familia maskini, alilipia ada wanafunzi ambao wazazi wao hawakuwa na uwezo, zaidi alitengeneza ajira nyingi kwa vijana. Hayo yalisababisha apendwe sana. Dudus aliitwa Rais wa Tivoli Gardens, alilindwa na kila mwananchi. Serikali ya Jamaica pia ilimlinda, maana alikuwa mfadhili wa viongozi. Marekani ilitaka Dudus akamatwe lakini Serikali ya Jamaica haikutekeleza. Dudus alipokamatwa na Marekani mwaka 2010, kwananchi wa Jamaica, hususan wakazi wa Tivoli Gardens, waliingia mitaani na kuandamana, wakitaka Dudus aachiwe huru. Wananchi walikuwa na mabango yaliyoandik

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AFUNGUKA HAYA KUHUSU KATIBA MPYA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale. Prof. Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.  Amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo. Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu, ili wazungumzie suala la Katiba Mpya. Hata hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na mwisho mzuri. CHANZO:UDAKU SPECIAL

Nape afunguka kwanini anaitwa Mkorofi

Image
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mbunge huyo wa Jimbo la Mtamba Nape Moses Nnauye amaeandika ujumb unaosomeka...  "Niliyashuhudia maisha haya mikoani (38months), nadhani ndio nikiyakumbuka naonekana mkorofi!!Iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu!‬" Facebook Twitter Google+ Pinterest Linkedin

Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema maisha yake yapo hatarini . Amesema "...pamoja na kuwa hawezi kulinganisha miaka saba iliyopita na sasa lakini bado maisha yangu hayako salama." akizungmza na Gazeti la MwanaHALISI, DkMwakyembe amesema " Siwezi kuwa salama siwezi kuwa naweza kutumia uhuru wangu wa kwenda kokote nikakota au wakati wowote ninaotaka. "kwamba naweza kutumia uhuru wangu huo kama unavyotakiwa. na katiba .... bado nina hofu ya maisha yangu ingwa siyo kama ilivyokuwa miaka ya mitano iliyopita " ameeleza DK Mwakyembe. DK Mwakyembe alikuwa ni mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya wanaotishiwa maisha. wengnie wanaotajwa kwenye orodhra hiyo  ni pamoja na Dr Willibrod Slaa. kauli ya Dk Mwakyembe imekuja siku tano baada ya watu wasiojulikana kumteka na  kumtesa mwanamuziki Ibrahim Musa Roma Mkatoliki. Dk Mwakyembe aliwahi kulipoti Februari Mwaka 2011 kuwepo kwa hatari ya kutokomeza miasha yake

MWANAMKE MWENYE SURA MBAYA DUNIANI

Image
Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani. Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye. Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie. Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''. Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi. Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo. Mwanamke huyo pia an

DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO

Image
Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja.   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.   Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo Moto Umeibuka katika duka kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda duka hilo lilianza kuungua majira ya 8:30. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. Magari ya zimamoto na uokoaji yalijazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne. Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana walikimbia nje ya duka kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi. Duka hilo kubwa la kisasa lenye yenye aina mbalimbali za bidhaa ni