DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO

Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja.

  Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.

  Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo



Moto Umeibuka katika duka kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda duka hilo lilianza kuungua majira ya 8:30. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana.

Magari ya zimamoto na uokoaji yalijazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.
Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana walikimbia nje ya duka kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.
Duka hilo kubwa la kisasa lenye yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na giza nene ndani ya jengo lililotawaliwa na wingu kubwa la moshi uliosababishwa na moto huo.
Waokoaji walijitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini changamoto ilikuwa kubwa kutokana na vikwazo vya giza na moshi mnene.

Comments

Popular posts from this blog