WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AFUNGUKA HAYA KUHUSU KATIBA MPYA
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale.
Prof.
Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya
Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la
Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao
wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba.
Amesema
kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo
utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo.
Aidha,
Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na
kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu,
ili wazungumzie suala la Katiba Mpya.
Hata
hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo
atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na
mwisho mzuri.
CHANZO:UDAKU SPECIAL
Comments
Post a Comment