Posts

MAJAMBAZI MANNE YALIYOUA ASKARI POSILI MKOANI PWANI YAUAWA NA POLISI

Image
Maafisa wa polisi wa Tanzania wamewaua watu wanne wanaoshukiwa kuhusika katika mauaji ya maafisa wanane wa polisi katika usiki wa Alhamisi kusini mwa mji wa Dar es Salaam. Kamishna wa polisi anayehusika na uchunguzi Nsato Mssanzya amesema katika mazungumzo na vyombo vya habari kwamba wanne hao walipigwa risasi muda mfupi Ijumaa alfajiri wakati wa msako. Maafisa waliouawa waliripotiwa kushambuliwa walipokuwa wakipiga doria katika mji huo. Kamishna huyo alisema kuwa bunduki nne zimepatikana kutoka kwa washukiwa waliouawa ikiwemo bunduki mbili zilizoibwa kutoka kwa polisi waliouawa, huku operesheni ya kuwasaka washukiwa waliosalia ikiendelea. Inspekta jenerali wa polisi Ernest Mangu alianzisha uchunguzi siku ya Alhamisi usiku. Tayari rais Magufuli ameshutumu mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanywa.

Wema Sepetu, Gabo wakinukisha

Image
Malkia wa filamu Wema Sepetu pamoja na Gabo Zigamba wataonekana kwenye filamu mpya ‘Heaven Sent’ inayoongozwa na Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment. Katika filamu hiyo Wema atakuwa kwenye mahusiano na Gabo Zigamba. “Sometimes in Life, You meet people for a Reason…. Im so happy I found the Reason I met you Gabo Zigamba #TheMaking of #HeavenSent,” aliandika Wema Instagram akiwa katika maandalizi ya kazi hiyo. Aliongeza, “Msichana naona mpaka mwaka kuisha watanzania watakuwa wameshaona uwezo wangu wa kubadilika wenye character tofauti. Nashukuru maana mpaka uchizi umenichezesha. Nashkuru sana binti Ndepanyaa.,” Stori pamoja na script ya filamu hiyo imeandaliwa na Neema Ndepanya.
Image
7 Tips to Make a Guy Fall in Love With You Love is a complicated thing. The chemistry of attraction is hard to pin down but it doesn’t stop people from falling in love. With every passing minute people meet, get married, start families, and create life-long partnerships. The force behind it all is simple: who would want to give up on love? We won’t have this beautiful world as it is if it wasn’t for love. People spend years waiting and searching for something true and pure. Sometimes it happens faster than expected – sometimes everything feels hopeless. No matter what you do: never give up on yourself and on finding love. We are here to help! 1.Be confident.....

Waliovunjiwa Nyumba Mkwajuni na Mkunguni Dar Kulipwa

Image
BUNGE limeelezwa kuwa wananchi waliovunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni ambao wana hati watalipwa fidia. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) aliyetaka kujua hatima ya watu waliovunjiwa nyumba katika eneo hilo. Naibu Waziri alisema, ni kweli watu walivunjiwa nyumba katika eneo la Mkwajuni na Mkunguni, hivyo wapeleke hati zao wizarani walipwe fidia. Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Salma Mwassa (CUF) aliyetaka kujua kuna umuhimu gani kusarisimisha nyumba alisema, kunapunguza migogoro ya ardhi. Mabula alisema urasimishaji wa ardhi maana yake ni kutambua miliki ya wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupimwa kisheria. Matokeo ya urasimishaji ni kutoa hati miliki na kuweka miundombinu ya msingi kama vile barabara, maji, mifereji ya maji ya mvua na ikiwezekana majina ya mitaa. “Urasimashaji ni mpango

skari Polisi 8 Wauawa na Majambazi.....Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi

Image
Ra i s wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi. Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. “Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. “Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimil

OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MAHESABU YA SERIKALI YAWASILISHA RIPOTI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA 2015/2016.

Image
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad na Mwenyeketi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka wakiangalia moja ya kitabu cha Ripoti kutoka Ofisi yake wakati alipokutana na na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma. Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AUSHANGAA UKIMYA WA MWIGULU NCHEMBA

Image
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anamshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuendelea kukaa kimya juu ya matatizo ya kiusalama kwa wananchi yanayoendelea nchini wakati yeye ndio kiongozi mwenye dhamana ya kulitatua hilo. Akiongea bungeni Jumanne hii, mbunge huyo amesema, “Kumekuwa na malalamiko mengi sana, tumeshuhudia malalamiko mengine yanahitaji majawabu kama siyo majibu ya haraka ili kuondoa hizi sintofahamu walizonazo wananchi.” “Niwaombe sana hakuna sababu ya mtu kama Mhe. Waziri Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao,” ameongeza. “Mimi binafsi niishauri serikali yangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali ya wasiwasi,” amesisitiza.

ISHU YA ROMA YAMFANYA DAVINA AMUUNGE MKONO WEMA SEPETU

Image
Halima Yahya ‘Davina’. BAADA ya supastaa wa filamu Wema Sepetu kuwashutumu wenzake wa Bongo Muvi kwa kutosapoti harakati za kupiga kelele kufuatia kupotea kwa Mwanamuziki wa Hip Hop, Ibrahimu Mussa ‘R.O.M.A’ kwa siku tatu na kusababisha kutoleana maneno makali mtandaoni na muigizaji mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’, Halima Yahya ‘Davina’ amemuunga mkono mrembo huyo wa zamani wa Tanzania akisema wapo wasanii ambao hawawasapoti wenzao wanapokuwa kwenye matatizo. Wema Sepetu. Akistorisha na Risasi Vibes, Davina alisema waraka alioandika na Wema kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba wasanii wa filamu hawana ushirikiano na wenzao hasa wanapokuwa katika matatizo ni kweli ingawa siyo wote. “Wema alichosema kipo Bongo Muvi, kuna watu hawana ushirikiano na wenzao, mimi huwa nawasapoti sana wenzangu, hata yeye alipokuwa Sentro nilikwenda kumuona, kwenye suala la ROMA karibu asilimia 50 ya wasanii waliposti katika kurasa zao,” alisema na kuwataka wasanii kushirik

BREAKING NEWS: Askofu Gwajima aachiwa huru na Mahakama. 0

Image
Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuchia huru Mchungaji wa kanisa LA Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima kufuatia kosa la Kutoa Lugha ya Matusi Dhidi ya Muadhama Polycap Kardinal Pengo mnamo mwaka 2015. Chini ya chini ya Hakimu mfawidhi Cyprian Mkeha Mahakama imeamuchia Askofu Gwajima kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya 225 ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Mbunge Hussein Bashe atumiwa ujumbe wa Vitisho, Usome hapa...

Image
Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo. Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka, “Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.” Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana. Vitisho hivi kwa mbunge huyo vimekuja ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu walipotekwa na watu wasiofahamika wakiwa katika studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MH. MAMA SAMIA SULUHU HASSAN APOKEA KIFIMBO CHA MALKIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kifimbo cha Malkia kutoka kwa bondia Haji Matumla, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kupokea kifimbo cha Malkia kuashiria uzinduzi wa michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Australia Aprili 2018, jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa kupokea kifimbo cha Malkia kuashiria uzinduzi wa michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Australia Aprili 2018, jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Haya ndio Majibu ya Halima Mdee kwa Gwajima

Image
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amejibu kile alichotuhumiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askafu  Josephat Gwajima kuwa anamuheshimu sana  mchungaji huyo. Mdee ameelza kwenye akaunti yake ya Twitwer kuwa hakumtukana Spika wa bunge na wala hatarajii kumtukana @halimamdee Namuheshimu sana Mch.Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.  https:// twitter.com/mitandaonblog/ status/851079630094299136  … 7:13 PM - 9 Apr 2017  ·  Dodoma, Tanzania     37 37 Retweets     204 204 likes  Follow Halima James Mdee   @halimamdee Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO.  https:// twitter.com/mitandaonblog/ status/851079630094299136  … 7:17 PM - 9 Apr 2017   ·   Dodoma, Tanzania

7 wasimamishwa kazi kwa ubadhirifu wa mil 900/-

Image
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imewasimamisha kazi watendaji waandamizi na wakuu wa idara saba wa manispaa hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha ya halamshauri hiyo ya Sh milioni 900. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo yamefanyika kupitia kikao cha fedha na uongozi cha halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Kigoma. Meya Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo ya kamati ya fedha na uongozi yametokana na taarifa ya mkaguzi wa ndani inayoonesha kuwepo kwa matumizi yanayotia shaka ya kiasi cha zaidi ya Sh milioni 900 ambazo maelezo yake na vielelezo vilivyopo vinatia shaka. Pamoja na hilo ametoa agizo kukamatwa na kuhojiwa kwa baadhi ya watalaamu kwa madai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha isivyo halali. Aliwataja waliosimamishwa kuwa ni pamoja na mhandisi wa ujenzi Boniface William, mhandisi msaidizi wa uj

MBUNGE WA JIMBO LA MTAMA MH. NAPE NNAUYE AZUNGUMZA NA WAZEE

Image
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao cha kati yake na wazee wa Mtama kikilchofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wazee wakati alipowasili katika ukumbi wa mkutano wake kati ya yake na wazee Mtama. Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na wazee wa Mtama leo kwenye ukumbi wa kianisa Katoliki Kijiji cha Majengo A. Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akifurahia jambo wakati akizungumza na wazee hao leo. Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye wakati akizungumzza nao leo. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mh. Nape nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake.

ABIRIA AJIFUNGUA MTOTO NDANI YA NDEGE FUTI 42,000 ANGANI

Image
Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES Wahudumu wa shirika la ndege la Uturuki wakiwa na mtoto aliyezaliwa Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana. Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso. Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINESI Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES  Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri. Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua. Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia k

ALICHOSEMA ROMA MKATOLIKI BAADA YA KURUHUSIWA KUTOKA POLISI

Image
Tangu zilipotoka taarifa kuwa ROMA Mkatoliki na wenzake watatu waliokuwa wamekamatwa na watu wasiojulikana wamepatikana wakiwa wazima Watanzania wengi wamekuwa na shauku ya kujua ni jambo gani kina ROMA wanaweza kuzungumza kuhusu tukio hilo. Baada ya kuruhusiwa na Polisi, ROMA amezungumza kwa ufupi kuhusu tukio hilo lakini akiwa hayupo tayari kuelezea kwa undani hadi pale watakaporuhusiwa na Polisi kwani kwa sasa taratibu za kiusalama haziwaruhusu kuelezea ni nini kimetokea.“Kwa kifupi tu niwahakikishe mimi ni mzima niko vema kabisa kiafya, kiakili na vinginevyo na hata wenzangu watatu nikimaanisha Mona, Bin Laden pamoja na Imma, tunaendelea vizuri na kwa sasa tupo katika taratibu za kutoa taarifa ya tukio zima, taratibu hizo zinatufunga tusiongee chochote kwa sasa hivi, “Ratiba ninayoweza kuwapa kupita kesho jumapili, siku ya jumatatu nadhani kutakuwa na press conference ya kuelezea habari nzima ilikuwaje, nawashukuru Watanzania wote sijapata nafasi ya kuingia

MZEE NDESAMBURO ALIVYOIPASUA CHADEMA KASKAZINI

Image
Wiki iliyopita kulikuwa na uchaguzi ndani ya Chadema ulilenga kuwapata viongozi wa Kanda ya Kaskazini lakini ukahirishwa ghafla na siku ya mwisho. Kuahirishwa kwa huo, licha ya kunaonekana kama ni tukio la kawaida kulizingira na mambo mengi yaliyojificha nyuma ya pazia. Chadema imekuwa ikiendelea na mipango yake ya kupanga safu za uongozi kwa kuzingatia sera yake ya kugatua madaraka ya chama kitaifa kwa ngazi za Kanda na wiki iliyopita ilikuwa zamu ya Kanda ya Kaskazini – yaani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambako uchaguzi huo ulikuwa ufanyike. Uchaguzi huo kulingana na vyanzo mbalimbali ndani ya chama hicho uliahirishwa kutokana na mvutano ulioibuka ndani ya Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi Tanga, baada ya kuwapo shinikizo la kutaka mwenyekiti wa Chadema Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo asigombee nafasi ya mwenyekiti wa Kanda. Ndesamburo ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Moshi mjini (2000-2015) alipoamua kutogombea, aliamua kuwania nafas