ABIRIA AJIFUNGUA MTOTO NDANI YA NDEGE FUTI 42,000 ANGANI

Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES
Wahudumu wa shirika la ndege la Uturuki wakiwa na mtoto aliyezaliwa
Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana.
Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso.Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.Haki miliki ya pichaTURKISH AIRLINESI Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege anganiHaki miliki ya pichaTURKISH AIRLINES 
Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani
Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri.
Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safariniMashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.

Comments

Popular posts from this blog