MAJAMBAZI MANNE YALIYOUA ASKARI POSILI MKOANI PWANI YAUAWA NA POLISI
Maafisa
wa polisi wa Tanzania wamewaua watu wanne wanaoshukiwa kuhusika katika
mauaji ya maafisa wanane wa polisi katika usiki wa Alhamisi kusini mwa
mji wa Dar es Salaam.
Kamishna
wa polisi anayehusika na uchunguzi Nsato Mssanzya amesema katika
mazungumzo na vyombo vya habari kwamba wanne hao walipigwa risasi muda
mfupi Ijumaa alfajiri wakati wa msako.
Maafisa waliouawa waliripotiwa kushambuliwa walipokuwa wakipiga doria katika mji huo.
Kamishna
huyo alisema kuwa bunduki nne zimepatikana kutoka kwa washukiwa
waliouawa ikiwemo bunduki mbili zilizoibwa kutoka kwa polisi waliouawa,
huku operesheni ya kuwasaka washukiwa waliosalia ikiendelea.
Inspekta jenerali wa polisi Ernest Mangu alianzisha uchunguzi siku ya Alhamisi usiku.
Tayari rais Magufuli ameshutumu mauaji hayo na kutaka uchunguzi kufanywa.
Comments
Post a Comment