MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AUSHANGAA UKIMYA WA MWIGULU NCHEMBA
Mbunge wa jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete anamshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
kuendelea kukaa kimya juu ya matatizo ya kiusalama kwa wananchi
yanayoendelea nchini wakati yeye ndio kiongozi mwenye dhamana ya
kulitatua hilo.
Akiongea bungeni Jumanne hii,
mbunge huyo amesema, “Kumekuwa na malalamiko mengi sana, tumeshuhudia
malalamiko mengine yanahitaji majawabu kama siyo majibu ya haraka ili
kuondoa hizi sintofahamu walizonazo wananchi.”
“Niwaombe sana hakuna sababu
ya mtu kama Mhe. Waziri Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi
wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao,” ameongeza.
“Mimi binafsi niishauri serikali yangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali ya wasiwasi,” amesisitiza.
Comments
Post a Comment