Posts

Mbunge Hussein Bashe aandika haya kuhusu Roma Mkatoliki

Image
 Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu” “Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Taifa letu kama Mzee Karume na Mwl Nyerere, Tunawajibu wa kukataa ukandamizaji

BREAKING NEWS:WATU WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI DAR NA MMOJA AFARIKI DUNIA

Image
Watu wanne wameripotiwa kufukiwa na kifusi  katika machimbo ya kokoto, Golani yaliyopo eneo la Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. DC wa Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wanahabari eneo la tukio. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa vyombo vya uokoaji vimefanikiwa kupata watu wawili ambapo mmoja alikuwa tayari amekwishafariki dunia. Mjema ameeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mtu wa pili  aliyeokolewa akiwa hai alikuwa amevunjika mguu ambaye pia amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa. Aidha DC Mjema ameeleza kuwa, wawili waliobakia hawajafanikiwa kuokolewa kutokana na changamoto ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha pamoja na ubovu wa miundombinu ya njia za kupitishia mitambo ya uokoaji. Eneo la machimbo hayo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salumu Hamdun

Hiki ndicho kilichofanya TID amuite Jide 'genious'

Image
Mbongo fleva ambaye amegoma kuitwa jina la TID na kupendekeza aitwe 'Mnyama' amekiri hewani kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa mkongwe wa muziki Bongo Lady Jadee ni 'genious' kwa kitendo cha kuwa na albam yenye jina kama la albam yake. Akiwa anaachia ngoma yake impya yenye jina la 'Woman' TID amesema wimbo wake huo aliutengeneza tangu mwaka uliopita hivyo hakuwa anajua kama mwana dada huyo ana albam inayofanana na jina la track yake. "Jide is a woman but mimi ni mwanaume ninayeimba kuhusu mwanamke. Huwezi amini kama mimi albamu yangu pia inaitwa Woman na kama Jide albamu yake inaitwa woman jua mimi ni hatari sana. Sasa kama mimi nina uwezo wa kufikiria kama Lady Jaydee basi mimi nitakuwa genious kufikiria kama lady Jaydee si kitu cha kitoto" Alisema TID Katika hatua nyingine TID amesema video yake ya Woman ni kazi ambayo imekuja kufanya mapinduzi kwenye kazi zake zote kwa sababu imegharimu dolla 12,000 (zaidi ya shilin

RAPA NAYA WA MITEGO NA ZITTO KABWE WAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA ROMA KUKAMATWA

Image
Baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva  Joseph Haule  ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop  Roma Mkatoliki  katika studio za  Tongwe Records  na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa. Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa  Nay wa Mitego  na Mbunge wa Kigoma Mjini  Zitto Kabwe  wameyaandika haya.. >>>” Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?!  Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.”  – Nay wa Mitego. >>>”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.”  – Zitto Kabwe.

Nape kuwaeleza ukweli wapiga kura wake jumamosi hii

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kusimamia haki huku akisema kuwa ataenda kuwaeleza wananchi wake ukweli wote. Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17,” ameandika Nape kupitia Twitter. Marchi 23, Rais Magufuli alimuondoa Nape kama Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria. 

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia. Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania). SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS ​ Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi. Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani. Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012. Siyo hiv

MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI

Image
Tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.  INDIRA Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.  JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani. LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.  THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika kufanya mauaji hayo ni rafiki yake wa k
Image
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai  ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA)  Halima Mdee  kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. Aidha Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi wa EALA. Pia Kamati ya Maadili leo imemuita DC Arumeru, Alexander Manyeti ambapo anatakiwa kutokeza mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa leo.

mwakyembe asema kuwa tukio la kuvamiwa clouds hawezi kulifumbia macho

Image
Dk. Mwakyembe aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kusitisha shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria hadi leo saa 3:00 asubuhi. Nipashe ilitaka kujua kinachoendelea kuhusu uchunguzi dhidi ya Makonda ambaye kamati ya watu watano iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ilitoa ripoti ikidai Mkuu wa Mkoa huyo alivamia kituo cha TV cha Clouds akiwa na askari wenye bunduki na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa kituo hicho. Kamati hiyo ilidai kubaini Makonda alifanya hivyo ili kulazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, irushwe hewani. Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki. Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatib

Wabunge wapania kumbana Kassim Majaliwa

Image
WABUNGE wa upinzani wamebainisha mambo manane ambayo wamepanga kumbana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atakapowasilisha makadirio ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge iliyotolewa Jumatatu na Ofisi ya Katibu wa Bunge, kikao cha leo ambacho ni cha tatu tangu kuanza kwa mkutano wa saba wa Bunge la 11, Waziri Mkuu atawasilisha makadirio ya bajeti yake. Wakizungumza na Nipashe nje ya Ukumbi wa Bunge jana, wabunge wa upinzani walibainisha mambo manane ambayo leo wangependa wapate ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mkuu wakati wa mjadala wa bajeti yake. Baadhi ya mambo hayo ni uchunguzi wa miili ya watu iliyoopolewa kwenye Mto Ruvu ikiwa imefungwa ndani ya sandarusi mwishoni mwa mwaka jana, utekelezaji wa kutoa Sh. milioni 50 kila kijiji, kusuasua kwa utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha, shughuli za serikali kuhamishiwa Dodoma na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora. KUFYEKWA BAJETI YA B

VIDEO: Halima Mdee alivyotumia neno "fala" "mpumbavu" Bungeni

Image
 T azama Video:

Chadema, CUF vyatinga Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi EALA

Image
Twaha Taslim aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki pia Mwanasheria wa CUF  VUGUVUGU la Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki wazidi kulitikisa bunge. tayati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama Cha Wananchi CUF vimepanga kutinga mahakamani kupinga matokeo hayo. Jana Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alitoa kauli ya kupinga matokea hayo mahakamani kutokana na kudai kuwa uchaguzi huo ulikwenda kinyume na taratibu za uchaguzi. Leo akizungumza na Muungwana Blog kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ahmed Katani, amesema kuwa uchaguzi huo umeendeshwa kinyume cha taratibu na kanuni za uchaguzi huo. Amesema kuwa jana majira ya saa 8 na dakika 37 kabla ya uchaguzi huo alipokea  barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Dk, Thomas Kashililah. Kwa mujibu wa barua hiyo ya Msimamiza wa uchaguzi ambayo alikiri kuwa kwa wagombea wa CUF kuna matatizo na kwamba hatuweza kushiriki kuchaguzi. Katani amesema aliandik

Mbowe amtuhumu Rais Magufuli, kwa jambo hili.

Image
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amtuhumu Rais John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika kwa alichodai kuwa ni kukeukwa kwa taratibu za uchaguzi. Mbowe ameongea hayo jana usiku mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa bunge  ambapo amedai kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Magufuli kuhusika kwenye mchakato wa kuyakataa majin ya wagombea wa Chadema. Mbowe amesema  kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro. Wagombea waliopendekezwa na Chadema  Wenje Na Masha kupigiwa kura za hapana katika  kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki Majina ya wagombea na matokeo KUNDI A: WANAWAKE 1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196 2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197 3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125 4. Ndg. Zainabu Ras

Jinsi Facebook ilivyohusika mkasa wa binti aliyejitosa baharini

Image
KISA cha binti mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa kutokana na miaka yake) kujitupa baharini akiwa katika boti ya Kilimanjaro V akitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar juzi, kinaanzia kwenye mawasiliano yake na mvulana mmoja, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, imefahamika. Msichana huyo alikuwa akiwasiliana na mvulana huyo ambaye walifahamiana kupitia Facebook, kwa kutumia simu ya mkononi. Nipashe ilifika Kikwajuni, nyumbani kwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu (shule inahifadhiwa) na kuikuta familia yake ikiwa na majonzi, huku wakiwa hawaamini kilichotokea na binti huyo akiwa bado hai. Akizungumza kwa huzuni, mama mdogo wa msichana huyo, Asha Saleh Mandhi, alisema palitokea mzozo baina yake na binti huyo baada ya kumkuta na simu ya mkononi wakati wazazi wake hawajamnunulia. Alisema Jumatano iliyopita majira ya jioni akiwa nyumbani hapo na baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake wa kumlea anamiliki simu, alimwita na

Washindi wa Bunge la Afrika Mashariki

Image
Wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki wamepatikana.