Chadema, CUF vyatinga Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi EALA
Twaha Taslim aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki pia Mwanasheria wa CUF |
VUGUVUGU la Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki wazidi kulitikisa bunge. tayati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama Cha Wananchi CUF vimepanga kutinga mahakamani kupinga matokeo hayo.
Jana Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alitoa kauli ya kupinga matokea hayo mahakamani kutokana na kudai kuwa uchaguzi huo ulikwenda kinyume na taratibu za uchaguzi.
Leo akizungumza na Muungwana Blog kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ahmed Katani, amesema kuwa uchaguzi huo umeendeshwa kinyume cha taratibu na kanuni za uchaguzi huo.
Amesema kuwa jana majira ya saa 8 na dakika 37 kabla ya uchaguzi huo alipokea barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Dk, Thomas Kashililah. Kwa mujibu wa barua hiyo ya Msimamiza wa uchaguzi ambayo alikiri kuwa kwa wagombea wa CUF kuna matatizo na kwamba hatuweza kushiriki kuchaguzi.
Katani amesema aliandika barua kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi huo Dk Kashililah aliyopinga majina ya walidaiwa kuwa wagombea wa CUF ambao hawakufuta tararibu ndani ya chama hicho,
Amesema kuwa Mohammedi hatibu Mnyea ambaye sio mwanachama chama hicho na alishafukuzwa kwenye chama, lakini pia mgombe mwengine ni Thomas Malima ambaye alijitoa jana ambapo kanuni zinasema kuwa mtu anatakiwa kujitoa siku tano kabla ya uchaguzi lakini pia mgombea huyo sio mwanachama wa chama hicho.
Pengamiz jengine ni juu ya Sonia Magogo ambaye ni Mwanachama ambaye hakufuata taratibu za uteuzi ndani ya CUF.
Katani amesema kuwa utaratibu ndani ya chama ni kikao cha Baraza kuu la Chama ndio lenye mamlaka ya uteuzi huo.
Amesema kuwa chama hicho kitaaenda Mahakamani siku ya juma tatu kupinga matokeo ya uchaguzi huo kabla ya kuapishwa kwa wabunge hao
Comments
Post a Comment