MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI
Tunawaletea
marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln;
alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington
kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na
mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.
INDIRA
Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa
kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New
Delh, India.
JOHN
Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963
mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi
barabarani.
LAURENT
Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na
watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.
THOMAS
Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa
miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika
kufanya mauaji hayo ni rafiki yake wa kisiasa Blaise Compaore
ambaye alikuja kuwa rais wa nchi hiyo kwa muda mrefu lakini
mwisho wa siku alikimbia nchi hiyo.
WILLIAM
Richard Tolbert Jr; Alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya
kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti
ndiye aliyetajwa kumuua.
MUHAMMAR
Muhamad Abu Migar al Ghaddaf; Alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42.
Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini
Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011.
ABEID
Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964.
Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye
hakuwahi kupatikana. Jean baptist ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa
mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara
ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye
kupinduliwa.
Comments
Post a Comment