Mbowe amtuhumu Rais Magufuli, kwa jambo hili.


MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amtuhumu Rais John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika kwa alichodai kuwa ni kukeukwa kwa taratibu za uchaguzi.

Mbowe ameongea hayo jana usiku mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa bunge  ambapo amedai kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Magufuli kuhusika kwenye mchakato wa kuyakataa majin ya wagombea wa Chadema.

Mbowe amesema  kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro.

Wagombea waliopendekezwa na Chadema  Wenje Na Masha kupigiwa kura za hapana katika  kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki

Majina ya wagombea na matokeo
KUNDI A: WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196

2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197

3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125

4. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM - KURA 137

KUNDI B: ZANZIBAR


1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME ME CCM - KURA 254

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA KE CCM - KURA 195

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH ME CCM - KURA 65

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI KE CCM - KURA 142


KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI

CHADEMA

1. Ndg. Ezekia Dibogo WENJE - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIYO 124 HAPANA 174

2. Ndg. Lawrence Kego MASHA - ME - CHADEMA - KURA ZA NDIO 126 HAPANA 198

CUF

1. Ndg. Habibu Mohamed MNYAA - ME - CUF KURA 188

2. Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO - KE - CUF KURA 06

3. Ndg. Thomas D.C MALIMA - ME - CUF- ALIJIONDOA

4. Ndg. Twaha Issa TASLIMA - ME - CUF KURA 140

KUNDI D: TANZANIA BARA

1.Ndg. Adam Omai KIMBISA - ME - CCM 266

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM 23

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM 81

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM 287

Wabunge saba ndio wamechaguliwa na nafasi mbili za CHADEMA bado zipo wazi.

WALIOSHINDA NI;

1. Fancy Haji Nkuhi

2. Happiness Elias Lugiko

3. Abdallah Hasnu Makame

4. Maryam Ussi Yahya

5. Habibu Mohamed Mnyaa

6. Ngwaru Jumanne Magembe

7. Adam Omary Kimbisa

Comments

Popular posts from this blog