BREAKING NEWS:WATU WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI DAR NA MMOJA AFARIKI DUNIA
DC wa Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wanahabari eneo la tukio.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa, tukio
hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa
mpaka sasa vyombo vya uokoaji vimefanikiwa kupata watu wawili ambapo
mmoja alikuwa tayari amekwishafariki dunia.
Mjema
ameeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili na mtu wa pili aliyeokolewa akiwa hai alikuwa
amevunjika mguu ambaye pia amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa.
Aidha
DC Mjema ameeleza kuwa, wawili waliobakia hawajafanikiwa kuokolewa
kutokana na changamoto ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha pamoja na
ubovu wa miundombinu ya njia za kupitishia mitambo ya uokoaji.
Eneo la machimbo hayo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salumu Hamduni amesema kuwa,
wanachokisubili mpaka sasa ni mtambo maalumu kwa ajili ya ukoaji.
Taratibu za kufukua miili ya watu iliyobaki ndani ya kifusi bado
inaendelea.
DC Sophia Mjema akitoa maelekezo, ambapo nyuma yake kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Suleiman Hamduni.
Comments
Post a Comment