Image result for ndugai
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Aidha Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi wa EALA.

Pia Kamati ya Maadili leo imemuita DC Arumeru, Alexander Manyeti ambapo anatakiwa kutokeza mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa leo.

Comments

Popular posts from this blog