RAIS MAGUFULI NA MWENYEKITI WA CCM AWAPA MAKAVU WALIOIMBA WANA IMANI NA LOWASSA MBELE YA KIKWETE
Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti. Akizungumza jana (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi . “Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea kuimba wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema. Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili katika kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.