VANESSA, DUMISHA HERI WAENDELEA KUSOTA POLISI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni
mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika
operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya
utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya
mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezwa na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi leo jijini Dar es Salaan.picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watuhumiwa
wawili wanaojihusisha usambazaji wa dawa kulevya pamoja na utumiaji wa
dawa hizo.
Wanaotuhumiwa
na usambazaji wa dawa za kulevya na utumiaji ni mwanamziki Vanessa Mdee
na Dumisha Heri ambao wamekamtwa na polisi hivi karibuni.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Polisi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon
Sirro amesema wasanii hao walikamatwa hivi karibuni katika mazingira
ambayo hakutaja kutokana na masuala ya kiupelelezi.
Amesema kuwa
baada ya kukamilika kwa upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili.
Wakati
huo huo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanaojihusisha na utapeli
kwa kutumia vicoba kuhusisha majina ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ,
Dk. Reginald Mengi ,Mke wa Rais Mstaa na Mbunge, Salma Kikwete pamoja
na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Amesema
kuwa matapeli hao wametengeneza mtandao wa Focus Vicoba ambao watu
wakiingia katika mtandao huo wanakuta taarifa mbalimbali zikiwemo za
viongozi na watu wenye uwezo wa kifedha kuwa ndio wanaoendesha Vicoba
hiyo kwa kutumia namba za simu za 0757 308381 na 0768 199359 ambazo sio
namba za viongozi hao.
Kamishina
Sirro amesema kuwa mwaka jana walimkamata Boniface Samson Ojwando (27)
kwa tuhuma za kuhusika katika matandao huo na kujipatia fedha kwa njia
za udanganyifu kwa mtandao wa kijamii.
Kamanda
Sirro amesema matapeli wengine walikuwa wanatumia gari zenye namba
usajili T 400 CNC aina ya Toyota Mark II Grand katika maeneo ya Sinza
kwa madai kuwa linauzwa baada ya na baada kukubaliana maziano hufanya
uhalifu wa kupora fadha hiyo iliotaka kununulia gari hilo.
Katika
hatua nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limekusanya
zaidi ya milioni 840 za makosa mbalimbali ya usalama Barabarani.
Comments
Post a Comment