RAIS MAGUFULI NA MWENYEKITI WA CCM AWAPA MAKAVU WALIOIMBA WANA IMANI NA LOWASSA MBELE YA KIKWETE

Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka
makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya
Halmashauri Kuu (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti.
Akizungumza jana (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema
kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na
kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi .
“Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti
makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona
hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea kuimba
wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema.
Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza
idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili
katika kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake
kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.

Comments

Popular posts from this blog