MTANGAZAJI DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM LEO
Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka.Kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani.Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile walichokuwa wanafanya. Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town.Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Kwefeee ukipenda Fetty siku ya kesho anadondoka mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja Xxl kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mje