Posts

MBUNGE PAULINA GEKUL APATAA AJALI MBAYA ALAZWA ICU

Image
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara. Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NA KUREJEA NCHINI KWAKE

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka    ma kurejea nchini kwake.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kuelekea kwenye ndege mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja w

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

Image
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi. Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo. Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo. Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, ameyasema hayo wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi. Dk. Kondo amesema, imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika

VIGOGO 4 WA SHIRIKA LA POSTA WATUMBULIWA

Image
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania, imetengua nafasi tatu za mameneja na ofisa mwandamizi kutokana na vitendo vya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea, ubadhirifu na wizi. Mameneja waliotenguliwa ni James Sando ambaye alikuwa Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali. Macrice Mbodo ameteuliwa kushika nafasi hiyo. Mwingine aliyetenguliwa ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara Janeth Msofe. Aliyekuwa Meneja wa Mkoa Shinyanga, Hassan Mwang'ombe kateuliwa kushika nafasi hiyo. Bodi pia imewasimamisha kazi Meneja Msaidizi wa Barua na Logistic, Jasson Kalile na Ofisa Mwandamizi wa Usafirishaji, Ambrose John. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, ameyasema hayo wakatia akizungumza na waandishi wa habari kuwajulisha uamuzi uliofanywa na bodi. Dk. Kondo amesema, imebainika na imewaridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa makao makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi na kujituma katika

RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKHRESA LEO JIJINI DAR

Image
  Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa    Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni    na    Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya K

RC MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA ATAJE MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya nne. Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa usiri. Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA). Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam. “Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama

HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOIZIMA YANGA UWANJA WA TAIFA

Image
Wachezaji wa Simba wakiwa wamembeba winga wa kulia wa timu hiyo Shiza Kichuya mara baada ya kuipatia Simba bao la ushindi katika mchezo wake wa ligi kuu ya Viodacom Tanzania Mameneja wa timu ya Simba wakiwa wamembeba mchezaji Shiza kichuya mara baada ya kuipatia timu hiyo bao la kuongoza katika mchezo wake dhidi ya Yanga Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekaa kwa huzuni mara baada ya timu yao kupigwa bao 2-1 na timu ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania. Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania. Kiungo wa kati wa Yanya Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka beki wa SimbaJanvier Bukungu Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka sawa mpira mbele ya beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondan Golkipa wa Yanga Deogratius Munishi akiokoampira uliopigwa na mshambualiaji wa Simba Laudit Mavugo Kiungo wa Simba Said Ndemla akiwania m

GARI LA MBUNGE LAUA, MWENYEWE ANUSURIKA

Image
Mtumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Moses Mjuni amefariki dunia baada ya kugongwa na gari la Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Esther Matiko katika Kijiji cha Kishamba wilayani humo.Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo alisema jana kwamba ajali hiyo ilitokea juzi saa mbili usiku, “Gari la mbunge lilimgonga mtumishi wetu wa Hospitali ya Magu ambaye alikuwa anaendesha pikipiki na dereva wa gari hilo amekamatwa yupo polisi,” alisema Nyembo. Akizungumza kwa simu jana, Matiko alisema ajali hiyo ilitokea takribani kilomita 10 kutoka Daraja la Mto Simiyu wakati akitoka Mwanza ambako walikutana na mwendesha pikipiki na dereva wake, Kelvin Matango alikuwa akimkwepa baada ya kuingia upande wake. “Nilitoka Mwanza saa 12:00 jioni kwenda jimboni kwangu (Tarime), tulipopita mbele kidogo karibu kilomita10 kutoka daraja la Mto Simiyu, ghafla alijitokeza mwendesha pikipiki akawa anaendesha kwa kuyumbayumba na dereva alishindwa jinsi ya kumkwepa akamgonga,

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI KATIKA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT JIJINI DAR

Image
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni wazir

MAHIGA ATOA SABABU ZA WATANZANIA KUFUKUZWA MSUMBIJI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo na akataka suala hilo lisiharibu mahusiano mapana yaliyopo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Balozi Mahiga alisema Tanzania imekuwa na ushirikiano na Msumbiji kwa muda mrefu hivyo utaratibu walioufuta wa kuwaondoa wahamiaji hao ni wa kiuungwana. Alisema jana mawaziri wa nchi 14 walianza kuwasili nchini kwa ajili ya kikao cha mawaziri ambacho Tanzania ni mwenyekiti wao, na siyo kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya Msumbiji, ila yenyewe ni nchi jirani na watazungumzia masuala ya ulinzi na usalma na ushirikiano wa nchi hizi za SADC. Alisema watu hao ambao waliingia Msumbiji bila kufuata taratibu, wakiwa huko pia wamevunja sheria za nchi hiyo kwa kujihusisha sh