MAHIGA ATOA SABABU ZA WATANZANIA KUFUKUZWA MSUMBIJI
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini
Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi
nchini humo na akataka suala hilo lisiharibu mahusiano mapana yaliyopo
ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Balozi Mahiga alisema
Tanzania imekuwa na ushirikiano na Msumbiji kwa muda mrefu hivyo
utaratibu walioufuta wa kuwaondoa wahamiaji hao ni wa kiuungwana.
Alisema
jana mawaziri wa nchi 14 walianza kuwasili nchini kwa ajili ya kikao cha
mawaziri ambacho Tanzania ni mwenyekiti wao, na siyo kwa ajili ya
kuzungumzia masuala ya Msumbiji, ila yenyewe ni nchi jirani na
watazungumzia masuala ya ulinzi na usalma na ushirikiano wa nchi hizi za
SADC.
Alisema
watu hao ambao waliingia Msumbiji bila kufuata taratibu, wakiwa huko pia
wamevunja sheria za nchi hiyo kwa kujihusisha shughuli bila vibali na
kinyume cha taratibu za ajira za nchi hiyo sanjali na kujiingiza katika
vitendo vya uhalifu mbaya.
“Watu
hawa wanajihusisha na biashara za madawa ya kulevya, silaha na
wanapokonya ajira za watu wa nchi hiyo... wahamiaji hao siyo Watanzania
pekee, bali na nchi zingine. Lililowagusa zaidi eneo hilo lina madini na
linafanana na Mererani na wameanza kufanya biashara hizo kinyume cha
Sheria na wameona raia wa Msumbiji hawanufaiki na biashara hiyo,”
alieleza.
Comments
Post a Comment