MBUNGE PAULINA GEKUL APATAA AJALI MBAYA ALAZWA ICU
Mbunge
wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari
lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya
ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira
Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa
babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia
katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika
kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa
babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua
umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari
kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
Comments
Post a Comment