RC MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA ATAJE MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja
hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni
kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu
ya nne.
Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka
watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu,
Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika
vifanyekazi zao kwa usiri.
Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja
watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka
tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya
Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi
semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar
es Salaam.
“Mzee
Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi
tukaona wacha tufanye kama alivyokuwa mnataka” alisema RC Makonda.
Aidha, RC Makonda amewakosoa wote
walioibuka na kumdhihaki sababu alitaja majina hayo akisema kuwa giza
haliwezi kuondolewa kwa giza bali ni kuwaleta waliopo gizani kwenye
nuru.
“Uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? Aliyefanya mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,” alisema Makonda.
Katika awamu ya tatu ya vita
dhidi ya dawa za kulevya, RC Makonda hakutangaza majina hadharani kama
alivyofanya katika awamu mbili zilizopita ambapo alimkabidhi majina 97,
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya
Rogers Sianga ili ayashughulikie.
Comments
Post a Comment