Posts

BREAKING NEWZZZZ…TRENI YA ABIRIA ITOKAYO KIGOMA KWENDA DAR YADONDOKA

Image
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani leo jioni Jumapili Januari 29, 2017. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa. Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo unmeaning na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio. “Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo

WALIOKWAMA KWENYE KIFUSI KWA SIKU MBILI KATIKA MGODI WA RZ NYARUGUSU WAOKOLEWA

Image
Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa asubuhi ya leo. Wachimbaji hao walikumbwa na kadhia hiyo, siku mbili zilizopita baada ya udongo kufunika sehemu ya kutokea. ila kwa juhudi mbalimbali walizokuwa wakizifanya, waliweza kuwasiliana na waliokuwa nje ya mgodi na hatimae kufanikiwa kuokolewa leo asubuhi. Baadhi ya Raia wa kigeni wenye asili ya China wakimjulia hali mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa walikumbwa na dhoruba hilo la kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita. Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo. Hivi ndivyo zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA KIKAO CHA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA A+ A- Print Email Share this PostFacebook shareTwitter sharePin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

Ten(10)Foolish Things to Say or Not to Say When Texting Boys

Image
We live at a time when most of our daily interactions happen through texts. That’s right, we rarely even call people anymore. We just text everyone. So it’s not surprising that a lot of our dating and flirting also happens through text. When you give a guy your phone number you don’t even expect him to call, you know he’ll text. It takes a bit of the pressure off, since you don’t have to speak your mind immediately, you can take your time and write out a perfect response. But texting boys can be tricky, there’s a balance you have to strike. That’s why we compiled a couple of pointers to help you figure out what you should and shouldn’t say when texting boys. 1. You never want to come off as clingy when texting a new boy . It might be a good idea to avoid texts like “I miss you”, and instead text him something like “ Wait till you see what I’m wearing” or “I can’t wait to take you home” . This way you’ll keep him interested and he’ll know you’re thinking of him.

Mwanamke Asimulia Alivyokuwa Akimshushia Kipigo Mumewe kwa Miaka 30 Mfululizo

Image
Mara nyingi vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia vimezoeleka kufanywa na wanaume dhidi ya wanawake na watoto. Hata hivyo, kampeni ya “Tunaweza” inayoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Kivulini jijini Mwanza kwa lengo la kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, imebaini kuwa vitendo hivyo pia hufanyika dhidi ya wanaume. Mkazi wa Mtaa wa Mwananchi, Kata ya Mahina jijini Mwanza, Ernest Kibinzaroya (78) ni mfano wa ukatili unaofanywa na wanawake dhidi ya wanaume. Yeye pamoja na mkewe, Maria Kibinzaroya (57) wamejitokeza hadharani kueleza walivyopitia maisha hayo. Inaelezwa kwamba Maria alikuwa akimpa kipigo cha mara kwa mara mumewe kabla ya ‘kuokoka’ na kuwa mke mwema. ‘Wokovu’ huo ni baada ya kampeni hiyo inayofanyika katika wilaya za Ilemela, Nyamagana, Magu, Misungwi, Sengerema mkoani Mwanza kuwafikia wanadoa hao na wote hivi sasa wana mabadiliko na wanapiga vita ukatili na unyanyasaji wa kijinsia. Akizungumza mbele ya mumewe wakati wa mahoji

BREAKING NEWS : KIONGOZI WA WALINZI WA IKULU YA GAMBIA ATOROKA

Image
Kamanda wa Polisi wa Jeshini (MP) katika ikulu ya Gambia, Luteni Nuha William Jammeh, yasemekana yupo mafichoni. Inasemekana alitoroka Gambia siku chache zilizopita. Kamanda huyu alitoa amri ya kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo walioonekana kumpinga Rais aliyemaliza muda wake, Yahya Jammeh. Kwa sasa Luteni Nuha Jammeh hajulikani alipo. Amekimbia mji mkuu wa Banjul na inaaminika kuwa amekimbilia nchini Senegal. Namba yake rasmi ya simu inayojulikana inaonesha kuwa yupo nchini Senegal ingawa simu yake imezimwa. Akimzungumzia Nuha Jammeh, mtu aliyewahi kusoma nae darasa moja alisema: ” Alikuwa mkimya sana na anayependa sana dini. Ilikuwa ni rahisi sana kuzoeana naye kipindi kile. Baada ya kukutana na Yahya Jammeh, huwezi jua, kwa maana yule dikteta alikuwa na uwezo wa kugeuza watu wazuri kabisa kuwa mashetani.”

KIPIGO CHA WANAJESHI CHA SABABISHA KIFO CHA KONDA WA DALADALA TANGA

Image
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini hapa. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.Mwananchi ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria. “Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid. Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEKAMATA MAGARI MATANO.

Image
Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro akizugumza na waandishi wa habari juu ya Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuhusu kukamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel massaka, Globu ya jamii. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha silaha aina ya SHORTGUN PUMP ACTON iliyo kutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huko Boko njiapanda leo jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano zilizokamatwa maeneo ya Hospital ya Mnazi mmoja jiji Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo. Pich

WAJIUA HUKU WAKIJIREKODI FACEBOOK

Image
Jay Bowdy (Kushoto) na Nakia Venant (Kulia).  MWANAUME mmoja nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Jay Bowdy, 34, ambaye pia ni muigizaji chipukizi amekutwa akiwa amejiua garini huku taarifa zikisema kwamba kabla ya kujiua, aliwaambia wafuasi wake kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook kwamba anajiua hivyo wawapigie simu polisi kutoka hapo Los Angeles na kuwaambia kwamba alikuwa akijiua.  Baada ya kupewa taarifa na raia wema, polisi kutoka katika kituo kikuu hapo Los Angeles walijaribu kumpigia jamaa aliyelipaki gari lake katika ya Mitaa ya Cumpston na Fulcher lakini hawakuweza kumpata kwa kuwa tayari alikuwa amekwishatekeleza kile alichokitaka.  Watu waliokuwa wakifuatilia tukio hilo katika video hiyo iliyokuwa ikirekodiwa ‘live’ walipigwa na bumbuwazi kwani wengi walihisi kwamba alikuwa akiigiza kutokana na kazi yake hiyo kumbe mshikaji alikuwa akijiua kweli. Baadaye video hiyo ikatolewa mtandaoni na Facebook.  SABABU YA KUJIUA  Chanzo kilichokuwa ha

JKCI KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI AFRIKA WA NCHINI MAREKANI WATOA HUDUMA YA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA

Image
Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Kulia ni Dkt. Peter Kisenge, akifuatiwa na Dkt. Peter O’brien na kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau. Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Madaktari Afrika wa nchini Marekani Dkt. Peter O’brien na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba bila ya kupasua kifua (Catheterization). Madaktari Bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari Afrika wa nchini Mare

ASKARI WAUA WATU 4 ARUSHA

Image
WATU wanne wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa ulinzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) huku mwanafunzi wa darasa la tatu anayesoma Shule ya Msingi Lemingori iliyopo Oldonyosambu wilayani Arumeru, Isaya Thomas (13) akiwa miongoni mwa majeruhi wa shambulio lililofanywa na askari hao. Kutokana na tukio hilo, Polisi inawashikilia askari sita wa Suma JKT kwa uchunguzi dhidi ya tukio hilo lililotokea Kijiji cha Kandaskirieti Kata ya Oldonyosambu Tarafa ya Mukulati huku miili ya watu wanne waliokufa kutokana na shambulio hilo, ikiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo akizungumzia tukio hilo, alisema juzi saa 11 jioni katika Kijiji cha Kandaskirieti, watu wanne walikufa baada ya kupigwa risasi na askari wa Suma JKT. Alisema taarifa za awali zimebaini kuwa askari hao wa Suma JKT ambao ni walinzi wa shamba la miti la serikali la Meru Usa Plant, walianza kufanya operes

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHAI CHA LUPEMBE NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe ikicheza ngoma ya Limdoya wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. Wasanii kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe wakicheza ngoma ya Limdoya wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wanyakazi Januari 25, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha chai cha Lupembe, Mussa Kefa (kushoto kwake) wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wafanyakazi akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. 

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI AWAMU YA KWANZA YA MIUNDOMBINU NA UTOAJI HUDUMA YA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe