WALIOKWAMA KWENYE KIFUSI KWA SIKU MBILI KATIKA MGODI WA RZ NYARUGUSU WAOKOLEWA



Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa asubuhi ya leo. Wachimbaji hao walikumbwa na kadhia hiyo, siku mbili zilizopita baada ya udongo kufunika sehemu ya kutokea. ila kwa juhudi mbalimbali walizokuwa wakizifanya, waliweza kuwasiliana na waliokuwa nje ya mgodi na hatimae kufanikiwa kuokolewa leo asubuhi.
Baadhi ya Raia wa kigeni wenye asili ya China wakimjulia hali mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa walikumbwa na dhoruba hilo la kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita.

Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo.
Hivi ndivyo zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji.


Comments

Popular posts from this blog