KIPIGO CHA WANAJESHI CHA SABABISHA KIFO CHA KONDA WA DALADALA TANGA
Kondakta
wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone,
Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya
kambi ya jeshi jijini hapa.
Kwa
mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati
akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado
kinachunguzwa.Mwananchi ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku,
ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi
na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui
Akizungumzia
tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari
hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua
zozote za kisheria.
“Tumekuwa
tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za
matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,”
alidai Khalid.
Diwani wa
Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji Mustapha
Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule moja
jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.
Comments
Post a Comment