JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEKAMATA MAGARI MATANO.
Kamishina
wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro akizugumza na
waandishi wa habari juu ya Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es
Salaam kuhusu kukamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa
katika vipindi tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel massaka, Globu ya jamii.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha silaha aina ya SHORTGUN PUMP ACTON iliyo
kutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huko Boko njiapanda leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano
zilizokamatwa maeneo ya Hospital ya Mnazi mmoja jiji Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika sehemu
mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu
ya Jamii
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha mitambo ya kutengenezea Gongo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionesha mkasi wa kuvunja.
Jeshi la
polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limekamata magari matano ambayo
yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo
mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es
Salaam CP Saimon Sirro amesema kuwa mnamo Januari 22 mwaka huu jeshi la
polisi lilikamata gari aina ya Toyota karina lenye namba za usajili T
950 DFN baada ya msako wa jeshi hilo katika maeneo ya Bandari jijini Dar
es salaam.
‘’Gari
jingine ambalo tumelikamata Toyota landcruseir Prado lenye namba
zasajili T 959 DFT gari hili katika uchunguzi wetu liliibiwa September
16 mwaka jana na badaye kuonekana maeneo ya Mwanza januari 21 Mwaka
huu’’ Alisema Kamishina Simon Sirro.
Kamishina
Sirro amesema kuwa jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa kwa wizi wa
pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es salaam na Pwani
pamoja na mkoa wa Morogoro baada ya operesheni iliyofanywa na jeshi hilo
.
Amesema
kuwa jeshi hilo limewakata vinara saba wa utengenezaji wa kadi bandia za
chanjo ya homa za manjano ambapo huziuza kwa watu wanaofika katika
hospitali ya Mnazi moja kwaajili ya kupata huduma za matibabu kabla
yakusafiri nje ya nchi.
‘’Baadhi
yawatuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na Aisha Hassani(29) mkazi wa
Vingunguti, Yakobo Msenga (42) mkazi wa Chanika, Oliver Bwegege
mhamasishaji (58) mkazi wa Kigogo’’ Ameongeza Sirro.
Comments
Post a Comment