Posts

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 15.12.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo Akamatwa na Polisi, Anyimwa Dhamana

Image
  DAR ES SALAAM: Mwanzilishi, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa selo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Police Central) leo Desemba 13, 2016. Polisi wameeleza muda huu kwamba leo atalala ndani (selo) hadi kesho atakapofikishwa mahakamani. Imeelezwa kuwa, kosa la kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni kukataa kutoa taarifa binafsi zilizohitajika za wateja wa mtandao anaoumiliki wa JamiiForums. Maxence ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa, kufanya hivyo ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi. Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari. CHANZO: JAMII FORUMS

MSANII CHUCHU HANS ASEMA HAYA BAADA YA KUSHINDA TUZO

Image
  Ushindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike wa Tuzo za EATV 2016 kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha mambo mengi aliyopitia kwenye maisha yake. Muigizaji huyo ambaye hakuwepo kwenye usiku huo wa tuzo na kuwakilishwa na meneja wake, ametoa ya moyoni kupitia Instagram kwa kusema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake. “Naamini kuna uwepo wangu kwa kila hatua tupigayo, ama hakika usitamalaki ya moyoni kwa kuyadhihaki ya machoni. Hii imenipa funzo zaidi ya lile alilonipa mama nikiwa na vunja ungo,” alisema Chuchu. “Mama aliniambia heshimu watu bila kuwa dhihaki kwa makundi,ama kuwa bagua kwa rika,” “Niwashukuru wote mlio nipigia kura amahakika mme tenda vema,likini mimi sio bora kuliko wenzangu ila nadhani kwa wino wakura zenu ulistahili niwe BEST ACTRESS, niwashukuru zaidi na zaidi, nikiandika maneno haya machozi yananitoka lakini hii yote ni heshima mlio nivika NENO LA KALE NI ASANTE,” aliongez

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Alichokisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kwenye Sherehe za Maulid, Singida

Image
Katika kusherekea siku ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammed (S.A.W), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali imani zao za kidini. Majaliwa ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida na kusema kuwa kuna matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika jamii na katika kuyachukulia hatua za kisheria vitendo hivyo Serikali haitakuwa ikibagua mtu kutokana na imani yake ya kidini kama jinsi inavyofanya kwa shughuli za maendeleo. “Serikali inawashukuru sana kwa kuendelea kuunga mkono jitihada ya Serikali ya Rais Magufuli, tunaamini juhudi tunazofanya za kuweka nidhamu kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi mtaendelea kutuunga mkono, tutaendelea kuruhusu uhuru wa kuabudu na kushirikiana na viongozi wa dini lakini tu mafundisho yanayotolewa yasikiuke sheria na kanuni za nchi, “Serikali ipo macho kupambana na tukio lolote lenye nia ya kupoteza amani ya

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. “Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema. “Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi

Meli Yenye Malori 600 ya Kiwanda cha Dangote Yawasili Mtwara

Image
MTWARA: Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dangote Cement Industries ya jijini Mtwara, ambaye pia ni bilionea namba moja Barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote jana Desemba 10, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini. Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana kuwa meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake mikoani, itawasili nchini. Aliongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini. Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo. Aidha, imeelezwa kuwa w

Baada ya Waziri Mkuu Majaliwa Kukabidhiwa Pembe, Mapya Tena Yaibuka Kifo cha Faru John

Image
Dar es Salaam. Kifo cha Faru John aliyehamishiwa Hifadhi ya Creta ya Ngorongoro kimeendelea kupunguza idadi ya wanyama hao ambao wanatafutwa kwa udi na uvumba na majangili kutokana na pembe zake kuuzwa ghali kwenye magendo, mara tatu zaidi ya dhahabu au dawa za kulevya aina ya cocaine. Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliliibua sakata la kutoweka kwa Faru John katika Hifadhi ya Sasakwa Black Rhino Sanctuary akidaiwa kufa. Kutokana na utata wa sehemu alipokuwa Faru huyo, makachero saba walifika Ngorongoro kufanya uchunguzi na kuwakamata maofisa watano waliotajwa kuhusika katika kumhamisha faru huyo. Hata hivyo, juzi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikabidhiwa pembe ikiwa ni kithibitisho kuwa Faru John amekufa. Pia, alipewa taarifa kuhusu utaratibu uliotumika kumhamisha kutoka Ngorongoro kwenda Sasakwa. Kilichosababisha Waziri Mkuu awe mbogo baada ya kuwapo kwa utata wa alipo faru huyo, ni upekee wake, thamani yake kiutalii na kuwa n

Mchungaji Awanywesha Waumini Dawa ya Kuua Bakteria “Dettol”

Image
MCHUNGAJI maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha  Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu. Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa. “Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”   – Mchungaji. Pia alisema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa “Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza m

Kamati Kuu ya CCM: Leo ni Kikao cha Kwanza kwa Mwenyekiti JPM, Yatakayojadiliwa Yapo Hapa

Image
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya CCM inakutana leo huku kaulimbiu ya “Hapa Kazi Tu” ikitarajiwa kutawala kikao hicho cha kwanza kwa mwenyekiti John Magufuli, ambaye ameonyesha dalili za kufumua sekretarieti wakati huu wa kuelekea uchaguzi wake mkuu. Kikao hicho cha siku mbili kitachofuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, pia kinatarajiwa kujadili mambo mengine nyeti, kama maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwakani kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa kwa kuchagua kamati Kuu mpya na suala la uchaguzi wa meya wa Kigamboni ambayo sasa ni wilaya. Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili chaguzi ndogo za mbunge wa Dimani na madiwani pamoja na ripoti ya wasaliti ambayo Magufuli alikabidhiwa na mtangulizi wake, Jakaya Kikwete Julai 23 baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti. Suala jingine linalotarajiwa kuchukua nafasi ni hali ya kisiasa nchini, ikijumuisha suala la Zanzibar, upigaji marufuku mikutano ya hadhara, hali ya kiuchumi ambayo inalalam