Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo Akamatwa na Polisi, Anyimwa Dhamana




jamii-forum 
DAR ES SALAAM: Mwanzilishi, Mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa selo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Police Central) leo Desemba 13, 2016. Polisi wameeleza muda huu kwamba leo atalala ndani (selo) hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.
Imeelezwa kuwa, kosa la kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni kukataa kutoa taarifa binafsi zilizohitajika za wateja wa mtandao anaoumiliki wa JamiiForums. Maxence ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa, kufanya hivyo ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi.
Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.
CHANZO: JAMII FORUMS

Comments

Popular posts from this blog