MTWARA: Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Dangote Cement Industries ya jijini Mtwara, ambaye pia ni
bilionea namba moja Barani Afrika, Alhaji Aliko Dangote jana Desemba 10,
2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu
jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda
chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza
hapa nchini.

Katika
kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana kuwa meli yenye
malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake mikoani, itawasili
nchini.

Aliongeza
kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida
pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo
hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana
nchini.

Baada
ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga
katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilipo.

Aidha,
imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye
malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.
Comments
Post a Comment