Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.
Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo
wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale
yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake
na kulewa.
“Kila mwandishi aliyeniandika
vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga
virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache
kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na
mnasikiliza tu,” alisema.
“Akisema Mungu uishi wewe basi,
nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza.
Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa
wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema
‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi nina
nguvu saaana,”alisema.
Hata hivyo baadaye mchungaji huo alishuka na kusema anamuachia Mungu wake ambaye atawahukumu kwa wakati wake.
“Lakini Mungu anasema tusihukumu, namuachia Mungu atawahukumu kwa wakati wake, haleluya, haleluya, Mungu awabariki sana.”
Novemba 24, mitandao ya kijamii
ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali
na jirani huyo ambaye anasikika sauti.
Taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo
wa kiroho zilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi
aliyeshuhudia tukio hilo, kuandika kwa urefu kisa hicho na kusambaza
kwenye mitandao ya kijamii.
Novemba 26, Mzee wa Upako kwa mara ya
kwanza alisita kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema
wanaomtuhumu waendelee kusema: “Sisemi, lakini siogopi kwenda jela
mimi na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni
kama kumpiga chura teke.”
Novemba 28, pia Mchungaji huyo akajibu
akisema maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo
matusi kwani yameandikwa kwenye biblia na kwamba watu hao ndiyo walianza
kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.
Jana, mchungaji huyo aliwahakikishia
waumini wake akisema waandishi walioandika kwa lengo la kumchafua
watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.
Katika mahubiri yake yaliyojengwa na
msingi wa Biblia kutoka kitabu cha Samweli wa kwanza, sura ya 16, mstari
wa saba, Mzee wa Upako aliyekaribishwa kwa nyimbo kadhaa ikiwamo
‘kusanya kusanya’ alisema yeye siyo mchungaji anayejikweza, lakini
baadhi ya wachungaji wakubwa kutoka nje wamekuwa wakienda kuomba upako.
Pia, alisema hata Rais John Magufuli hakumuita yeye bali aliona kitu ndani yake na kubarikiwa kabla ya kumtembelea.
TUZO YA FILAMU BORA YA MWAKA EATV AWARDS ILIYOCHUKULIWA NA CHUCHU HANS
Comments
Post a Comment