Posts

Mongela Atinga Mitaani Kuhimiza Usafi wa Jiji la Mwanza

Image
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akikatiza katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza usafi. Mhe. John Mongela akitoa maelezo kuondoa vitu vilivyowekwa nje ya duka la mkazi wa Mwanza. Wakazi wa Mwanza eneo la soko kuu wakiondoa uchafu katika mtaro uliopo eneo hilo. Mwananchi huyu akiondoa takataka zilizopo kwenye mtaro uliopakana na duka lake.    Zoezi la kusafisha Jiji la Mwanza likiendelea. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ametembea mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza kuhimiza watu kufanya usafi katika maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kutoa muongozo wa namna wafanyabiashara watakavyoendesha biashara zao. Ziara hiyo imefanyika baada ya kumaliza zoezi la kuondoa wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika maeneo yasiyoruhusiwa na kuwapeleka maeneo mbalimbali ambayo yalitengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao. Katika ziara hiyo iliyokuwa imeambatana na viongozi mbalimbali wa serikali walipita maeneo ya Makoroboi, Liber

Trump Kusitisha Uagizwaji wa Ndege Mpya za Air Force One

Image
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani. Wiki sita kabla ya kuchaguliwa, aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa: “Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 billion. Futa oda hiyo!” Serikali ya Marekani iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing ili kutengenezwa kwa ndege hizo mbili au zaidi za kuwabeba marais. Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024. Hisa za kampuni ya ndege ya Boeing zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trumpp kwenye Twitter, ingawa zilijikwamua baadaye. Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili wa mwaka 2020.

Serikali Kuanzisha Tuzo za Mitandao ya Kijamii kwa Wanahabari

Image
Mwandishi wa habari wa mtandao huu, Denis Mtima (kushoto) akikabidhiwa kadi ya kujiunga na mfuko wa hiari wa mwanachama wa PSPF na Waziri Nape Nnauye. Nape akimkabidhi mwanadada mwandishi wa habari, kadi ya ATM ya NMB. …Akisisitiza jambo fulani kwa wanahabari. …Akizungumza jambo. Mwakilishi wa wadhamini wa semina hiyo ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo, akizungumza jambo kwenye hafla hiyo. Mkurugenzi wa mfuko wa hiari wa mwanachama wa PSPf, Adam Mayingu ambao nao walikuwa wadhamini wa semina hiyo, akizungumza jambo. Vicky Bishubo akimkabidhi Nape zawadi iliyokuwa imeandaliwa kutoka NMB. Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo. WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema serikali inatarajia kuanzisha Tuzo za Umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs na website) kuanzia mwakani 2017. Hayo ameyasema jana wakati akifunga semina kwa mtandao wa wamiliki wa mitandao ya kijamii

Waziri Mkuu Majaliwa Ataka Nyaraka za Faru John Ifikapo Kesho

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameugiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro (NCAA), kumpelekea nyaraka zote zilizotumika katika kumhamisha faru maarufu kwa jina la John katika hifadhi hiyo ifikapo Desemba 8, 2016. Majaliwa amesema ana taarifa kuwa walimhamisha Faru John Kreta kwa siri na kumpeleka  V I P Grumet  Serengeti Disemba 17, 2015 na waliahidiwa kupewa sh. milioni 200 ambapo  na wamepewa sh.  milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni 100 nyingine baadaye. Amesema hayo Desemba 6, 2016 alipotembelea Ofisi za makao makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha  wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa  Baraza la Wafugaji ikiwa ni  sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa. “Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itath

Diamond na Zari Wamepata Mtoto wa Kiume Leo Des. 6, Bofya Hapa Kuona Pichaz

Image
Pretoria, Afrika Kusini: TAARIFA njema kwa mashabiki wa msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, Nasbu Abdul “Diamond Platnumz” ambaye leo leo Desemba 6, 2016, mpenzi wake Zarina Hassan “Zari The Boss Lady” amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Netcare iliyopo mjini Pretoria nchini Afrika Kusini. Mtoto aliyekuwa akisubiliwa kwa hamu kubwa. k Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Diamond kupitia ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya Instagram ameeleza kuwa mtoto wao huyo amezaliwa majira ya saa 8:35 usiku kwa saa za Afrika kusini ambazo ni sawa na saa 10:35 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki. Mbali na Diamond kuposti picha zikionesha miguu ya mtoto huku akieleza kuwa mpaka sasa bado hawajapata jina la kumuita mtoto wao, mpenzi wake, Zari ameposti picha ikionesha mikono ya kichanga chao na kuwashukuru wale wote waliokuwa wakimuombea kwa Mungu ili ajifungue salama. Mtoto huyo anakuwa ni wa pili kwa Diamond kuzaa na mpenzi wake Zari baada ya m

Ajali ya Lori na Hiace Yaua Watu 9 na Kujeruhi 18, Iringa

Image
   IRINGA: Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana Desemba 5, 2016 baada ya lori kugongana na gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.   Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema dereva wa lori lililopata ajali lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara.   “Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika vibaya,” alisema RC Masenza.   “Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambayo ilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu.”  RC Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine. “Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema RC Masenza.

Zari Kujifungua Soon, Apelekwa Hospitali Sauz, Diamond na Mama Yake Waungana Naye

Image
   HABARI ya town kwa sasa ni kuhusu kujifungua kwa mpenzi wa mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz, Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond anayetarajia kupata mtoto wa kiume ametupia video inayomuonesha Zari akiwasili katika hospitali ambayo haikutajwa jina iliyopo nchini Afrika Kusini ikionyesha dhahiri kwamba yupo tayari kujifungua mtoto wa pili wa nguli huyo wa Bongo Fleva ambapo aliandika ni Jina gani vile mmesema nimpe? Zari alikuwa kwenye kiti cha kubebea wagonjwa “Wheel Chair” wakati akifikishwa hospitalini hapo huku pembeni akiwepo mama mkwe wake, Sandra Kassim ambaye ni mama mzazi wa Diamond pamoja na wahudumu wa hospitali hiyo. Mapema leo, staa huyo aliweka picha yake akiambatana na mama yake mzazi wakiwa kwenye ndege wakielekea Afrika Kusini kwa ajili ya kuwa karibu na Zari huku akiandika maneno yafuatayo; Na mama Chibu D Chibu De … flying to our new Second home, South africa For my

PICHA: SAFARI YA MWISHO YA FIDEL CASTRO WA CUBA

Image
Mwili wake wa aliyekuwa Rais wa Cuba umechomwa moto hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya kibinafsi, na majivu yake yamezungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago leo Desemba 4, 2016. Cuba inaadhimisha siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel Castro akiwa na umri wa miaka 90. Kasiki lenye majivu ya Fidel Castro yakiwekwa garini tayari kwa kuzungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Kasiki lenye majivu ya Fidel Castro yakiwa garini kuzungushwa katika msafara maalumu kote nchini Gari maalumu likiwa na Kasiki lenye majivu ya Fidel Castro yakiwa garini kuzungushwa katika msafara maalumu kote nchini Wananchi wakijipanga kuaga Kasiki lenye majivu ya Fidel Castro yakiwa garini kuzungushwa katika msafara maalumu kote nchini Cuba.

Ndege mpya ya ATCL yapata hitilafu uwanja wa ndege Arusha

Image
Ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jana ilipata hitilafu katika uwanja wa ndege wa jijini Arusha hali iliyopelekea ndege hiyo kushindwa kuendelea na ratiba kama ilivyokuwa imepangwa. Taarifa kutoka katika uwanja wa ndege wa Arusha zinaeleza kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilipata pancha ikiwa katika barabara ya kurukia ndege. Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa tairi moja ya ndege hiyo lilitoka nje ya barabara ya ndege kukimbilia wakati ndege hiyo ilipokuwa inatua uwanjani hapo hivyo ikakwama kwenye nyasi. Chanzo cha ndege hiyo kutoka nje ya barabara ya kukimbilia ndege kimeelezwa kuwa ni wembamba wa barabara hiyo kiasi kwamba rubani akikosea kidogo tu, basi ndege hutoka nje. Hadi sasa Shirika la Ndege la Tanzania halijatoa taarifa yoyote kuelezea tukio hilo.

Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushtukiza Gereza la Ukonga Dar

Image
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2016        Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza, John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2016 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016. Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea  na